Nenda kwa yaliyomo

Fotoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fotoni (ing. photon, kutoka gir. φῶς, φωτός fos,fotos nuru) ni sehemu ndogo ya chini kabisa ya usafirishaji wa nishati ya nuru (mwanga) kwa njia ya vifurushi au kwanta.

Nadharia ya kwanta inaeleza kwamba aina zote za nishati husafirishwa kutoka eneo moja hadi jingine kwa viwango vidogovidogo (vifurushi/kwanta).

Kwa upande wa nuru kiwango hicho kidogo kabisa huitwa fotoni.

Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fotoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.