Nenda kwa yaliyomo

John von Neumann

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
John von Neumann
John von Neumann baada ya 1940
John von Neumann baada ya 1940
Alizaliwa 28 Desemba 1903 Budapest
Alikufa 8 Februari 1957 Washington, D.C.
Nchi Marekani
Kazi yake Mtaalamu wa hisabati

John von Neumann (28 Desemba 1903 - 8 Februari 1957) alikuwa mtaalamu wa hisabati nchini Marekani. Alizaliwa Budapest kama mtoto wa familia ya Wahungaria wa Kiyahudi aliyeonekana mapema kuwa na akili bora. Baada ya kumaliza shule alisoma uhandisi Berlin na Zürich akaendelea na msomo ya hisabati. Tangu 1926 alikuwa mwalimu na baadaye proofesa wa hisabati kwenye vyuo vikuu vya Berlin na Hamburg. 1930 alihamia Marekani alipokuwa profesa kwenye chuo kikuu cha Princeton.

Anahesabiwa kati ya wanahisabati muhimu zaidi ya karne ya 20. Hisabati yake yalisaidia kuelewa fizikia ya kwanta na kwa hiyo alishiriki katika kazi za kuanzisha bomu ya nyuklia wakati wa vita kuu ya pili ya dunia.