Nenda kwa yaliyomo

Ufunda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ufunda
Kundi la ufunda tumbo-njano (Ostorhinchus apogonoides)
Kundi la ufunda tumbo-njano (Ostorhinchus apogonoides)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Perciformes (Samaki kama ngege)
Familia: Apogonidae (Samaki walio na nasaba na ufunda)
Günther, 1859
Ngazi za chini

Jenasi 37 na spishi 362, 50 katika Afrika ya Mashariki:

Funda, dagaa-donzi au dagaa ya gege ni samaki wadogo kiasi wa baharini wa familia Apogonidae katika oda Perciformes lakini spishi kadhaa zinaishi katika maji baridi, zile za jenasi Glossamia hasa.

Kwa kawaida funda ni samaki wadogo. Spishi nyingi huwa chini ya sm 10 na mara nyingi huwa rangi kali. Wanajulikana kwa mdomo wao mkubwa na kwa mgawanyiko wa pezimgongo katika mapezi mawili tofauti. Spishi nyingi huishi katika maji ya tropiki au nusutropiki, ambapo hukaa katika miamba ya matumbawe na nyangwa. Hawa ni samaki wa usiku na wanashinda mchana katika mianya ya giza ndani ya mwamba. Angalau baadhi ya spishi huatamia mayai yao ndani ya mdomo wa madume.

Spishi za Afrika ya Mashariki

[hariri | hariri chanzo]
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ufunda kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.