Timothy Fosu-Mensah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Timothy_Fosu-Mensah

Timothy Fosu-Mensah (alizaliwa 2 Januari 1998) ni mchezaji wa soka raia wa Uholanzi ambaye anacheza kama kiungo mkabaji au beki wa klabu ya Manchester United, na timu ya taifa ya Uholanzi.

Kazi ya klabu[hariri | hariri chanzo]

Crystal Palace (mkopo)[hariri | hariri chanzo]

Mnamo tarehe 10 Agosti 2017, Fosu-Mensah alijiunga na Crystal Palace kwa mkopo wa muda mrefu.Alicheza katika timu hiyo siku mbili baadaye mnamo tarehe 12 Agosti dhidi ya Huddersfield Town, wakifungwa magoli 3-0.

Fulham (mkopo)[hariri | hariri chanzo]

Mnamo tarehe 9 Agosti 2018, Fosu-Mensah alijiunga na klabu ya Fulham kwa mkopo wa muda mrefu.Alicheza mechi yake ya kwanza na klabu hiyo mnamo 18 Agosti 2018 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye Ligi Kuu, akicheza dakika 90 kamili yaani mechi nzima.

Kazi ya kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Alicheza katika mashindano ya chini ya miaka 16, na baadaye tena aliiwakilisha uholanzi katika mashindano ya chini ya miaka 19 , Fosu-Mensah alipewa tuzo kwa kuichezea Uholanzi na wito wake wa kwanza wa kwenda katika timu ya wakubwa katika mechi ya kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Ireland na zinginezo kama Poland na Austria.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Timothy Fosu-Mensah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.