Teopempto na Teona

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kifodini chao.

Teopempto na Teona (walifariki 304) ni Wakristo waliofia dini yao huko Nikomedia (leo nchini Uturuki) wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian.

Teotempto alikuwa askofu wa mji huo, Teona alikuwa mchawi aliyeitwa kummaliza baada ya njia nyingine ya kumuua kushindikana. Kumbe, alipoona dawa zake pia hazikumweza, alikubali kubatizwa naye. Hatimaye Teotempto alikatwa kichwa na Teona alizikwa akiwa hai[1][2][3].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Januari[4] au 5 Januari.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Serbian Orthodox Church - The Hieromartyr Theopemptus and the Holy Martyr Theonas. Iliwekwa mnamo 19 April 2018.
  2. Hieromartyr Theopemptus the Bishop of Nicomedia (5 January 2008). Iliwekwa mnamo 19 April 2018.
  3. Hieromartyr Theopemptus the Bishop of Nicomedia. Iliwekwa mnamo 19 April 2018.
  4. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.