Tanzanaiti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kito cha Tanzanaiti katika hali asilia
Tanzanaiti baada ya kukatwa na kung'arishwa

Tanzanaiti ni kito chenye rangi ya buluu hadi dhambarau na kijani. Inachimbwa katika kaskazini ya Tanzania.

Tanzanaiti iligunduliwa mara ya kwanza mwaka 1967 katika milima ya Mererani karibu na mji wa Arusha. Kito hiki inapendwa sana kimataifa bei zake zilicheza kati ya dola za Marekani 250 na 500 kwa karati moja (=milligramu 200).

Kikemia ni aina ya madini ya Zoiziti ambayo haina thamani kubwa vile katika maumbo mengine. Lakini tanzanaiti bandia inatengenezwa kwa kupasha moto fuwele za zoiziti ya kawaida zinazobadilika rangi motoni.