Nenda kwa yaliyomo

Tambarazi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tambarazi
Tambarazi madoadoa
Tambarazi madoadoa
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Certhioidea (Ndege kama tambarazi)
Familia: Certhiidae (Ndege walio na mnasaba na tambarazi)
Ngazi za chini

Jenasi 2 na spishi 11:

Tambarazi ni ndege wadogo wa familia Certhiidae. Wana rangi ya kahawia au kijivu na madoa au michirizi nyeupe mgongoni na nyeupe chini. Domo lao limepindika na linatumika ili kutafuta wadudu chini ya gome. Tambarazi madoadoa ni spishi pekee ya Afrika kwa kweli. Inatokea Uhindi ya kaskazini pia. Huko Afrika ya Kaskazini kuna nususpishi ya tambarazi wa Ulaya: tambarazi kaskazi.

Tambarazi hula wadudu tu. Tambarazi madoadoa hulijenga tago lao kwa umbo la kikombe juu ya tawi la mlalo na hulificha chini ya kuvumwani, mavi ya viwavi na tandabui. Spishi nyingine hulijenga tago lao kwa umbo la kikombe juu ya vijiti vilivyokwama kati ya gome na shina. Jike huyataga mayai 3-9.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine

[hariri | hariri chanzo]