TAKILUKI
Jump to navigation
Jump to search
TAKILUKI (au TAKILUKIZA) ni kifupi cha Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Zanzibar. Taasisi hii ilianzishwa mwaka wa 1979. Inafanya kazi chini ya udhamini wa wizara ya elimu Zanzibar
Majukumu ya TAKILUKI[hariri | hariri chanzo]
- Kufundisha Kiswahili kwa wageni mbalimbali wanaofika Zanzibar
- Kufanya utafiti kuhusu lahaja mbalimbali na fasihi simulizi ya Kiswahili
- Kutoa mafunzo na masomo ya Kiswahili kwa watumishi wa Serikali, viongozi mbalimbali na wageni ili kukuza ujuzi wao wa lugha ya Kiswahili kwa ujumla na kuwawezesha kutumia Kiswahili fasaha.
- Kutoa mafunzo ya lugha za kigeni kwa watu mbalimbali.
- Kukusanya na kuchambua fasihi simulizi ya visiwa vya Unguja na Pemba.