Chechele (Stenostiridae)
Mandhari
(Elekezwa kutoka Stenostira)
Chechele | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Chechele buluu
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 4, spishi 9:
|
Chechele ni ndege wa familia Monarchidae na Stenostiridae. Zamani wale wa Stenostiridae waliainishwa katika familia Muscicapidae (Culicicapa), Monarchidae (Elminia), Sylviidae (Stenostira) na Rhipiduridae (Chelidorhynx), lakini uchunguzi wa ADN umeonyesha kwamba wana mnasaba na kwa hivyo wamepewa familia yao.
Wana rangi ya buluu (Elminia), ya kijivu (Stenostira) au ya manjano (Chelidorhynx na Culicicapa). Wanatokea misituni au porini kwa vichaka katika Afrika na Asia. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe katika panda ya matawi. Jike huyataga mayai 2.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Elminia albicauda, Chechele Mkia-mweupe (White-tailed blue flycatcher)
- Elminia albiventris, Chechele-kishungi Tumbo-jeupe (White-bellied crested flycatcher)
- Elminia albonotata, Chechele-kishungi Mkia-mweupe (White-tailed crested flycatcher)
- Elminia longicauda, Chechele Buluu (African blue flycatcher)
- Elminia nigromitrata, Chechele-kishungi Mweusi (Dusky crested flycatcher)
- Stenostira scita, Chechele Kinyago (Fairy flycatcher)
Spishi za Asia
[hariri | hariri chanzo]- Chelidorhynx hypoxantha (Yellow-bellied fantail)
- Culicicapa ceylonensis (Grey-headed canary-flycatcher)
- Culicicapa helianthea (Citrine canary-flycatcher)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Chechele mkia-mweupe
-
Chechele-kishungi mkia-mweupe
-
Chechele kinyago
-
Yellow-bellied fantail
-
Grey-headed canary-flycatcher
-
Citrine canary-flycatcher