Saruji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Simiti)
Kiwanda cha saruji

Saruji (pia: simiti, simenti) ni mata laini kama ungaunga unaotengenezwa kutokana na mawe chokaa, udongo wa mfinyanzi, mchanga, chuma na mengine. Kwa kawaida huonekana kama unga wa rangi ya kijivu.

Hukorogwa na maji kuwa na hali kati ya ujiuji ila baada ya muda inaanza kuganda na kuwa imara kama jiwe.

Saruji imekuwa muhimu sana katika shughuli za ujenzi. Awali ilitumiwa kwa kushika mawe au matofali ya ukuta vikae pamoja.

Baadaye ikagunduliwa ya kwamba saruji ikichanganywa na mchanga ma mawe madogo (kama kokoto) kuwa zege inaweza kumwagwa kati ya bao mbili na kuwa imara ndani yake. Kwa njia hiyo imewezekana kujenga haraka sana kwa kumwaga mchanganyiko wa zege ya saruji katika nafasi zilizoandaliwa awali. Hapo nondo za chuma zinaingizwa ndani ya ukuta au sakafu ya saruji kwa kusudi la kuongeza uimara.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.