Nenda kwa yaliyomo

Siku ya Ushairi Duniani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtu akighani shairi

Siku ya Ushairi Duniani husherehekewa kila mwaka tarehe 21 Machi.

Ilipitishwa rasmi na shirika la Umoja wa Mataifa la UNESCO (Shirika la Elimu, sayansi na utamaduni) mnamo mwaka 1999 ili "kuunga mkono lugha tofauti kupitia ushairi na kuongeza fursa ya kuziokoa lugha zilizo hatarini kusikiwa na kuziokoa kupitia ushairi".[1]

Malengo ni kuhamasisha usomaji, uandishi, uchapishaji na ufundishaji wa mashairi duniani, kama linavyosema azimio la UNESCO "kutoa utambuzi mpya na msukumo kwa harakati za kitaifa, kikanda na kimataifa".

Kwa kawaida siku hiyo husherehekewa katika mwezi March, lakini pia katika nyakati hizi jumuia nyingi zilianza kuisherekea katika tarehe 15 Oktoba wakati wa kuzaliwa kwa Virgil, mshairi katika Roma ya Kale. Utamaduni wa kuisherekea siku hiyo katika mwezi Oktoba bado unaendelea katika nchi nyingi.[2] Nchini Uingereza siku hiyo huadhimishwa katika Jumatano ya kwanza ya mwezi Oktoba, katika sehemu nyingine huadhimishwa tofauti na mwezi wa Oktoba na wengine huadhimisha katika mwezi Novemba.

  1. "World Poetry Day, 21 March". www.un.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-11-10.
  2. 41 countries observed World Poetry Day on 15 October 1951. Ref. cited: The International Who's Who in Poetry 1978-79. Ernest Kay, Ed. International Biographical Council, Cambridge, England.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Siku ya Ushairi Duniani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.