Mathias E. Mnyampala
(Elekezwa kutoka Mathias Mnyampala)
Mathias E. Mnyampala (Muntundya Ihumwa, Wilaya ya Chamwino, mkoa wa Dodoma, 18 Novemba 1917 - mjini Dodoma, 8 Juni 1969) alikuwa mwanasheria, mzalendo wa Taifa la Tanzania na lugha yake Kiswahili, mwandishi na mshairi maarufu.
Kufuatana na maoni ya Profesa Madumulla, Mathias E. Mnyampala sasa hivi nchini Tanzania ni Jabali Lililosahaulika. Utafiti wa Vyuo Vikuu vya Tanzania na ng'ambo, hasa Ufaransa, haukukaa kimya kuhusu kazi yake upande wa Ushairi wa Kiswahili na Historia ya Wagogo wa Tanganyika. Lakini bado matokeo yake yanahitaji kuenezwa.
Vitabu vichache vya Mathias E. Mnyampala[hariri | hariri chanzo]
- Mnyampala, M. E. (1954). Historia, mila, na desturi za Wagogo wa Tanganyika. Eagle Press.
- Mnyampala, M. (1962). Utenzi wa Enjili Takatifu. Ndanda Mission Press.
- Mnyampala, M. E. (1963). Diwani ya Mnyampala (Vol. 5). East African Literature Bureau.
- Mnyampala, M. E. (1970). Ngonjera za ukuta. Oxford University Press.
- Shihabdin Chiraghdin na Mathias E. Mnyampala (1977). Historia ya Kiswahili. Oxford University Press.
- Mnyampala, M. E. (1995). Maddox, G. H. The Gogo: history, customs, and traditions. ME Sharpe Inc.
- Mnyampala, M. E. (2011). Historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi (1924-1964). Ahmadiyya Printing Press. Dar es Salam. Tanzania. ISBN 9789976891645. 109 p.
- Mnyampala, M. E. (2013). Maisha ni kugharimia. DL2A - Buluu Publishing. France. ISBN 9791092789027. 112 p.
- Mnyampala, M. E. (2014). Ugogo na ardhi yake. DL2A - Buluu Publishing. France. ISBN 9791092789201. 112 p.
Kujua zaidi kuhusu Mathias E. Mnyampala[hariri | hariri chanzo]
- Madumulla, J. S. (2011). Mathias Eugene Mnyampala (Jabali Lililosahaulika).
- Mulokozi, M. M., & Sengo, T. S. (1995). History of Kiswahili poetry. TUKI/Inst. of Kiswahili Research.
- (fr) Roy, Mathieu, & Mnyampala, Charles M. (2007). Picha yake Mathias E. Mnyampala. http://medihal.archives-ouvertes.fr/medihal-00517208/
- (fr) Roy, Mathieu (2013). MATHIAS E. MNYAMPALA (1917-1969): POÉSIE D'EXPRESSION SWAHILIE ET CONSTRUCTION NATIONALE TANZANIENNE (Doctoral dissertation, Institut National des Langues et Civilisations Orientales-INALCO PARIS-LANGUES O'). Anwani yake kwa Kiswahili: Mathias E. Mnyampala (1917-1969): Ushairi wa Kiswahili na Ujenzi wa Taifa la Tanzania. Tasnifu ya PhD.
- (fr) Ukurasa wa Mathias E. Mnyampala katika wikipedia.fr Mathias E. Mnyampala
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
![]() |
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mathias E. Mnyampala kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |