Siku ya Matendo Mema
Siku ya Matendo Mema ni siku ya kimataifa ya kujitolea iliyoanza mwaka 2007. Siku hiyo hufanyika kila mwaka katika mwezi wa Machi au Aprili.
Lengo ni kuunganisha watu wengi duniani kwa ajili ya kufanya matendo mema kwa wengine na kwa ajili ya dunia.
Siku hiyo ya huduma za kijamii ilizinduliwa mara ya kwanza nchini Israel na mfanyabiashara mwanamke mhisaniShari Arison, kupitia Ruach Tova, ambayo ni asasi isiyo ya kifaida ambayo inaunganishwa watu wanaotaka kijitolea pamoja na taasisi nyingine. Kuzungumzia kuhusu siku hii, Shari Arison amesema: 'Ninaamini kwamba kama watu wote watafikiri mambo mema, kuzungumza mema na kutenda mema, mzunguko wa kutenda mema utaongezeka duniani, siku ya matendo mema imekuwa siku yenye muhamko mkubwa wa utoaji wa matumaini, na mwaka huu watu binafsi, watoto wa shule, wanajeshi na wafanyakazi kutoka katika shughuli nyingi mbalimbali wanaungana kwa ajili ya siku ya matendo mema ya mwaka, kwa ajili ya kufanya matendo mema kwa wengine kama kumbukizi' [1].
Historia
[hariri | hariri chanzo]Katika Israeli
[hariri | hariri chanzo]Siku ya Matendo (kwa Kiyahudi: יום המעשים הטובים) ilianza mwaka 2007. Kwa makadirio ya watu wapatao 7,000 walishiriki nchini Israel katika mwaka huo.
Hadi mwaka 2016 walifikia watu 1,500,000. Kampuni mbalimbali zikishiriki pamoja na asasi zisizo za kifaida nchi nzima kwa kuandaa shughuli mbalimbali za kijamii, kama vile kupaka rangi majengo, kupanda bustani za kijamii pamoja na mambo mbalimbali yanayohitajika katika jamii, miji kama Tel Aviv na Yerusalemu ziliandaa matamasha maalumu ya wazi.
Uungwaji mkono na Dunia
[hariri | hariri chanzo]Kufikia mwaka 2011 dunia nzima ilianza kushiriki ikijumuisha Marekani, Ukraine na Poland. Mwaka 2011, kampuni za kimataifa Shikun & Binui na Bank Hapoalim zilikuwa miongoni mwa kampuni za kwanza ya kimataifa kushiriki katika siku ya matendo mema nje ya Israeli, siku ya matendo mema imekuwa ikisherehekewa katika miji mikubwa kama Roma, São Paulo, Kaohsiung City, na New York City kwa kuandaa matamasha maalumu. Katika siku hiyo katika eneo la Herald Square, New York City, msanii na mwigizaji Adrian Grenier aliunga mkono kwa kuzungumza katika siku ya tamasha
ni muhimu kuwa na siku ambayo itawafanya watu kuyafikiria zaidi kufanya mammbo mazuri .[2]
Mwaka 2012, mpango huu uliungwa mkono na MTV na kufanya kampeni ya wiki sita katika runinga yake ya mtandaoni, na ujumbe kuwafikia zaidi ya watu milioni 24 duniani.
Papa Fransisko akishiriki siku ya matendo mema 2015 mjini Roma alisema:
nina tuma ujumbe wangu kwa wote wanaojitolea kuwa wanapaswa kuungana na kuonyesha utu wa kufanya mambo mazuri ili kuitengeneza jamii iliyo bora.[3]
Mwaka 2016 siku ya matendo mema nchini Brazil walifikia watu 10,000 nchi nzima, na miji 40 ya Brazili ikijumuisha miji mikubwa kama Rio de Janeiro, Brasília, na São Paulo.
Katika Amerika ya Kilatini, tukio kubwa lilifanyika Panama, Costa Rica, Brazil, Peru, na nchi nyingine 16.
Huko Taiwan, siku ya matendo mema iliungana na TAVE (Taiwan Association for Volunteer Effort) kufanya shughuli kubwa katika miji mikubwa ya Kaohsiung City, Taiwan 2016. Makamo wa Raisi, Chen Chien-jen, na Kaohsiung’s Mayor, Chen Chu, walikuwa miongoni wa wageni wa heshima waloshiriki siku hii.[4] Taoyuan City ulisherehekea siku hii , na kuandaliwa na Taoyuan City Volunteer Service Association na asasi nyingine shiriki.[5]
Mwaka wa 2020 ni mwaka wa 14 wa siku ya matendo mema, kwa makadirio zaidi ya nchi 93 zitashiriki na jumla watu 2,500,000 watajitolea duniani, siku hii husherehekewa na nchi kama Kenya, Tanzania, Ureno, Italia na nchi nyingine.
Siku ya matendo mema na Ruach Tova ni sehemu ya Ted Arison Family Foundation, na mhisani wa Arison Group.
Tarehe
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Tarehe ya Israeli | Tarehe ya kimataifa |
---|---|---|
2007 | Mei 8 | N/A |
2008 | Machi 24 | N/A |
2009 | Machi 25 | N/A |
2010 | Machi 16 | N/A |
2011 | Aprili 5 | Aprili 5 |
2012 | Machi 20 | Machi 25 |
2013 | Machi 3 | Machi 10 |
2014 | Machi 11 | Machi 9 |
2015 | Machi 24 | Machi 15 |
2016 | Machi 15 | Aprili 10 |
2017 | Machi 28 | Aprili 2 |
2018 | Machi 13 | Aprili 15 |
2019 | Aprili 2 | Aprili 7 |
2020 | Machi 24 | Machi 29 |
2021 | Machi 16 | Aprili 11 |
2022 | Machi 29 | Aprili 3 |
2023 | Machi 21 | Aprili 16 |
2024 | Aprili 9 | Aprili 14 |
2025 | Aprili 1 | Aprili 6 |
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]SIku ya Matendo Mema imepokea tuzo ya George W. Romney Affiliate Excellence Award ya 2016.[6]
Tazama Pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 900,000 people take part in Good Deeds Day (Israel21c)
- ↑ Adrian Grenier speaks in the 2016 Good Deeds Day Event at Herald Square, New York City (Youtube)
- ↑ "Pope honors Good Deeds Day (Shari Arison)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-08-11. Iliwekwa mnamo 2020-03-08.
- ↑ (TaiwanHot, in Chinese)
- ↑ "(Now News, in Chinese)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-07-03. Iliwekwa mnamo 2020-03-08.
- ↑ Good Deeds Day won the 2016 George W. Romney Affiliate Excellence Award (PR Newswire)