Siku ya Wanawake Duniani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa tarehe 8 Machi ya kila mwaka. Siku hiyo ilianza kuadhimishwa tarehe 8 Machi 1975 baada ya Umoja wa Mataifa kuridhia siku hii kutumika [1] kama siku rasmi ya kuikumbusha dunia juu ya haki za wanawake.Siku hii pia huongeza chachu katika harakati za mapambano katika usawa wa kijinsia kwa wanawake na wanaume katika jamii. Aidha maadhimisho ya siku hiyo kwa mwaka huu yamebeba ujumbe wa usawa kwa watu wote.

Historia

Siku ya wanawake duniani kwa mara wa kwanza ilisherehekewa katika mwaka wa 1911 ambapo mataifa kumi na moja yalikusanya wanawake mia moja walipoanza kuadhimisha siku hii.

Mwaka 1908 jumla ya wanawake elfu kumi na tano waliandamana katika katika mji wa New York wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi ,kupata ujira wa kuridhisha na kupewa haki ya kupiga kura [2].

Mwaka 1909 mwanamke kwa jina la Clara Zetkin alipendekeza kuanzishwa kwa siku ya wanawake duniani katika mkutano wa wafanyakazi wanawake uliofanyika katika jiji la Copenhagen nchini Denmark.

Marejeo