Siku ya Mandela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nelson Mandela mwaka 2008
Wafanyakazi wa MONUSCO wakifanya usafi katika hospitali ya Goma, kusherehekea siku ya Mandela 2012.

Siku ya kimataifa ya Nelson Mandela (au Siku ya Mandela) ni siku ya kimataifa kwa heshima ya Nelson Mandela, sikukuu hii ambayo husherehekewa kila mwaka tarehe 18 Julai, siku ya kuzaliwa ya Mandela kama sehemu ya kutambua mchango wake kwa jamii za Afrika ya Kusini, na Afrika kwa ujumla na ulimwengu wote.[1]. Siku hiyo iliteuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa mnamo Novemba mwaka 2009,[2] na kwa mara ya kwanza siku hiyo iliadhimishwa tarehe 18 Julai mwaka 2010, lakini, makundi mengine yalianza kusherehekea siku hiyo tarehe 18 Julai mwaka 2009.

Tarehe 27 Aprili mwaka 2009, 46664 na Nelson Mandela Foundation ilizialika Jumuia za kimataifa kuungana kwa ajili ya sherehe maalumu ya siku ya Mandela.[3] Siku hiyo haimaanishi ni siku ya mapumziko, lakini humaanisha ni siku ya heshima kwa Mandela, rais na mpigania uhuru wa Afrika ya Kusini. Thamani yake ni kujitolea kwa ajili ya huduma za kijamii.[1][4]

Siku ya Mandela ni kwa ajili ya kuiambia dunia ichukue hatua za kimabadiliko na kusherehekea mawazo ya kuibadili jamii katika uwezo wa kuleta nguvu ya mabadiliko. Ujumbe katika Kampeni ya Mandela ni:

"Nelson Mandela amepigania haki za kijamii kwa miaka 67. Tunakuomba ufanye hivyo ndani ya dakika 67."[5] "Tutakuwa watu wenye heshima kama tutaileta dunia pamoja kupambana na umaskini, kunadi na kuitangaza amani, kukataa ubaguzi na kuendeleza utamaduni bora," kulingana na mambo bora ya Mandela.[6]

Kwa mara ya kwanza siku hiyo ilisherehekewa tarehe 18 Julai mwaka 2009, wakati wa siku ya kuzaliwa ya Nelson Mandela, ukiwa ni muendelezo wa kielimu, sanaa za maonyesho, harambee na matamasha ya kujitolea yaliyoandaliwa na kuongoza tamasha katika Radio City Music Hall iliyoandaliwa na tamasha la 46664 pamoja na the Nelson Mandela Foundation.[5] mwezi November 2009, the Mkuitano mkuu wa Umoja wa Mataifa ulikubali kuwa 18 July iwe ni "Siku ya kimataifa ya Nelson Mandela".[7]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Nelson Mandela International Day, July 18, For Freedom, Justice and Democracy. un.org. Iliwekwa mnamo 11 July 2011.
  2. "Resolution adopted by the General Assembly", General Assembly, United Nations, 1 December 2009.
  3. The Nelson Mandela Foundation and 46664 call for the establishment of a global ‘Mandela Day’ – Nelson Mandela Foundation (en-us).
  4. "46664 and the Nelson Mandela Foundation Call for Establishment of Global 'Mandela...", Reuters, 27 April 2009. Retrieved on 31 July 2010. Archived from the original on 2013-02-01. 
  5. 5.0 5.1 Mandela Day. Mandela Day. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-03-11. Iliwekwa mnamo 31 July 2010.
  6. "World urged to mark 'Mandela Day'", BBC News, 27 April 2009. Retrieved on 1 April 2010. 
  7. "UN gives backing to 'Mandela Day'", BBC News, 11 November 2009. Retrieved on 16 November 2009. 

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]