Shura

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Shura (kwa Kiingereza: saltpeter) ni kundi la chumvi za nitrati zinazotokea kiasili.

Kikemia ni nitrati zifuatazo zilizoitwa shura au saltpeter:

  • Nitrati ya kalisi KNO3
  • Nitrati ya sodiamu NaNO3
  • Nitrati ya kalisi Ca(NO3)

Matumizi kwa baruti[hariri | hariri chanzo]

Shura ilikuwa sehemu ya lazima ya mchanganyiko wa dutu unaounda baruti. Tangu kugunduliwa na kuenea kwa baruti na silaha za moto katika karne ya 12 shura ilitafutwa kwa madhumuni ya kijeshi.

Shura hiyo ilikuwa kwa kawaida nitrati ya kali KNO3 iliyopatikana katika aina za ardhi[1], katika mavi ya ndege au katika mipango ambako iliweza kuonekana kama chumvi juu ya mwamba[2] . Katika nchi ambako haikupatikana katika mazingira, wataalamu walibuni njia za kuitengeneza kwa kukusanya mkojo wa wanyama, hata ya watu[3].

Mbolea wa chumvichumvi[hariri | hariri chanzo]

Elimu ya kemia ya kisasa ilitambua elementi ndani ya shura; kuanzia mwaka 1840 mwanakemia Justus Liebig alifundisha kwamba ustawi wa mimea shambani unahitaji kurudishwa kwa madini kwenye ardhi ambayo yanatolewa na mimea yenyewe inapokua. Hapo aliweka msingi wa matumizi ya mbolea za chumvichumvi yaliyokuwa msingi wa kuongezeka kwa mavuno duniani yanayolisha idadi kubwa ya watu[4] .

Shura za aina mbalimbali zilionekana kuwa na virutubisho vya msingi vinavyohitajika na mimea yaani naitrojeni (N) na potasiamu (K).

Shura ya NaNO3 inapatikana kwa viwango vikubwa katika Amerika Kusini, hasa katika jangwa la Atacama. Tangu kugunduliwa kwa umuhimu wa mbolea za chumvichumvi shura hiyo ilitafutwa sana na kufanyiwa biashara kimataifa; utajiri huo ulisababisha "vita ya shura" ya karne ya 19 baina ya Chile, Peru na Bolivia kuhusu utawala wa maeneo ynye shura nyingi.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Ahmad Y Hassan, Potassium Nitrate in Arabic and Latin Sources Archived 2008-02-26 at the Wayback Machine, History of Science and Technology in Islam.
  2. Major George Rains (1861). Notes on Making Saltpetre from the Earth of the Caves. New Orleans, LA: Daily Delta Job Office. uk. 14. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo July 29, 2013. Iliwekwa mnamo September 13, 2012.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  3. Joseph LeConte (1862). Instructions for the Manufacture of Saltpeter. Columbia, S.C.: South Carolina Military Department. uk. 14. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-10-13. Iliwekwa mnamo 2007-10-19.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
  4. Commercial fertilizers increase crop yields [1]. Accessed 9 April 2012.