Nenda kwa yaliyomo

Shule ya Lenana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lenana School
Location
Nairobi, Kenya
Coordinates 1° 18' 0.957" S, 36° 43' 41.775" E [1]
Information
Type National, Public
Motto Nihil Praeter Optimum
Established 1949
Head teacher Mr. P. W. Warui
Number of students 1030
Campus Karen, Nairobi
Color(s) Maroon and Grey
whiterose
Sare ya Renana

Shule ya Lenana ni shule ya upili mjini Nairobi, Kenya. Ilianzishwa mwaka wa 1949 na gavana wa kikoloni, Philip Euen Mitchell; wakati huo shule hii ilikuwa inajulikana kama Duke of York School . Mwalimu mkuu wa kwanza alikuwa RH James.

Shule hii ilipoanzishwa ilikuwa ya wanafunzi wazungu pekee ndani ya mfumo wa kikoloni wa rangi wa Kenya. Walimu wote (mabwana, kama walivyoitwa wakati huo), pia walikuwa wazungu. walikuwa watoto wa walowezi kutoka Uingereza, ambao wengi wao walikuwa wakulima katika maeneo karibu na shule. Hii ilihitaji kwa kimsingi mabweni kwa wanafunzi, ingawa awali kulikuwa wanafunzi wachache ambao walikuja kila siku na kurudi nyumbani siku ikiisha. Mfumo wa Lenana ulikuwa unafanana na ule mfumo wa shule za umma za Kiingereza.

Kufikia mapema miaka ya 1960 shule ilikuwa imemalizika kikamilifu kwani ilikuwa na kozi yake ya shimo 9 ya mchezo wa gofuf, mchezo wa kutumia bunduki kulenga mbali (rifle range), farasi wengi, na ardhi kubwa ya michezo kama vile kriketi, raga, kandanda, mpira wa magongo, kuogelea, tenisi, boga, na michezo mingine. Klabu cha unajimu vile vile kilkuwa na darubini, madarasa za sayansi zilikuwa na vifaa mbalimbali na vizuri vya shule na vifaa vingine vya shule vilitumika kusailing, kupanda mlima na mengineyo. Shule ilikuwana maji yake kutoka visima, na kifaa cha kutibu taka majini. Wafanyikazi walikuwa wanaishi ndani ya shule kampasi na wao ndio walioona ustawi wa Kitivo na wanafunzi. Wafanyikazi hawa walifanya kazi ya usafi, ufuaji nguo, upishi wa vyakula, misingi ya kutunza eneo za shule na kazi zinazofanana, hivyo basi kuwaacha wanafunzi na uhuru wa kusoma na kujifunza pamoja na shughuli za burudani.

Kenya ilipopata uhuru mwaka wa 1963 kulikuwa na mabadiliko yaliyopelekea wanafunzi wachache wa kwanza Waafrika na WaHindi kuingizwa katika shule hiyo katikati ya miaka ya 1960. Wanafunzi hawa wa kwanza walibaguliwa kirangi lakini wao ndio waliofungua milango kwa Wakenya wengine kuwafuata kuingia katika skuli hiyo. Walimu Waafrika waliaza kuajiriwa mwanzo wa miaka ya 1970 na pia wao hawakuepuka ubaguzi wa kirangi ambao ulifanya kazi iwe ngumu.

JIna la shule lilibadilishwa na kuwa Lenana School (katika muktadha huu tutatumia jina shule ya Lenana) mwaka wa 1967. Mwalimu mkuu wa kwanza kutoka Kenya alikuwa James Kamunge.

Shule ya Lenana wakati huu ilikuwavna wanafunzi 1200. Mwaka wa 2006, shule hii ilikuwa katika nafasi ya 26 katika orodha ya shule za upili bora nchini Kenya kufuatia matokeo ya mtihani wa kitaifa wa Kenya Certificate of Secondary Education. Kupitia miaka ya 1990 na kuingia katika karne ya 21, Shule ya Lenana imeimarisha viwango vya juu vya elimu.

Wito wa Shule

[hariri | hariri chanzo]
  • Nihil Praeter Optimum, Latin for 'Nothing But The Best'

Wimbo wa Shule

[hariri | hariri chanzo]

Thoughts and deeds shall bide with task.
Keep the Rose brightly ye our emblem.
Sieve the trash dear Lord we ask.
For Nihil Praeter Optimum.
In pride we ride.
With rules abide.
As all the boys and staff combine.
All members here in Lenana.
We aim at Nothing But The Best.

Shule ya Lenana inajumuishwa kama shule ya Kitaifa. Hii inamaanisha kuwa wanafunzi wake ni wale waliofanya vizuri katika mtihani wa kitaifa wa Kenya Certificate of Primary Education (KCPE). Malengo yake ya kuchagua wanafunzi yamaanisha kwamba kila darasa la wanafunzi linaloingia ni kubwa na limewakilishwa kutoka kote nchini. Madarasa yanayofunzwa yanajumuisha sayansi zote kamili na sanaa pamoja na madarsa ya ujuzi wa kimaisha kwa wanafunzi ambao wanahamu ya kujifunza. Mtaala unaweza kufikiriwa kuwa mzito kwa upande wa sayansi lakini makini pia inatiliwa katika mafunzo ya utu kupitia madarasa hayo na kuhakikisha kuwa mwanafunzi anafaidika kuwa mwanafunzi mwenye ujuzi zaidi ya moja na uzoefu huu unamfanya mwanafunzi awetayari kukumbana na maisha baada ya shule. Mara kwa mara shule hii hufanya vyema kitaifa katika mitihani ya Kenya Certificate of Secondary Education (KCSE) na mfululizo huwa katika nafasi za juu katka orodha ya shule zenye wanafunzi. Wanafunzi wanaohitimu kutoka Shule ya Lenana huendeleza masomo yao na kupata kazi tofautitofauti.

Shughuli nyinginezo

[hariri | hariri chanzo]

Kwa kuwa hii ni shule ya bweni, shughuli nyinginezo kucheza sehemu kubwa katika maisha ya kila siku ya mwanafunzi. Hadi mwisho huu, hakuna uhaba wa shughuli ambazo wanafunzi wanaweza kujitupa ndani wenyewe. Baadhi ya shughuli hizi zimewekwa katika mtaala na hivyo basi kuna muda wa kumaliza shughuli hizi. Kazi ya Kijamii imeundwa ndiposa kumwezesha mwanafunzi aweze kujua umuhimu wa mazingira kuwa safi. Kimsingi shughuli hizi ni kama kazi za usafi zinazofanywa mapema asubuhi isipokuwa Jumapili. Wanafunzi pia hushiriki katika shughuli za kuigiza. Kuna mashindano kati ya majumba katika maigizo, muziki na kila aina ya michezo ambayo yanachukuliwa kwa umakini sana kwani kutoka kwa mashindano haya ni wawakilishi wa shule huchaguliwa kushindana nje.

Kuna idadi kubwa ya vilabu mbalimbali ambavyo hupatia wanafunzi fursa ya kuungana na wanafunzi wengine, ndani na nje ya shule. Mifano ya vilabu hivi ni pamoja na klabu ya Jumuiya ya Madola (zamani ilikuwa klabu ya Umoja wa Mataifa), klabu ya Kifaransa, klabu ya Rifle, klabu ya Skauti, klabu ya Duma (hii ni klabu ya viranja) na klabu ya Umoja wa Kikristo, na hizi ni chache tu. Mara kwa mara, shule ya Lenana huwa mwenyeji wa sherehe (zinazojulikana kama funkies) tofauti, wageni waalikwa wakiwa wanafunzi kutoka shule zingine zilizo karibu na mbali. Sherehe hizi ni pamoja na sherehe au mashindano ya Uigizaji, sikukuu au mashindano ya muziki, kongresi ya Sayansi na mengine mengi. Magazeti ya shule ya Lenana pia ni shughuli maarufu, pamoja na barua rasmi ya shule inayojulikana kama Laibon ama yenye kusengenyana kama vile Scandal, Peep nk.

Changez (kama Shule ya Lenana inavyojulikana sana) ina njia inayotumia kuwachukua wanafunzi kutoka kila pembe ya nchi. Hii ina maana kwamba kuna shughuli mbalimbali za michezo kama walivyo wanafunzi wa asili tofauti. . Wanafunzi wengi huja katika shule ya Lenana wakiwa hapo awali wameshiriki katika michezo na kwa wale ambao hawana historia ya michezo hujihusisha katika michezo hii baadaye. Kutokana na ukubwa wa idadi ya wanafunzi, kuna tabia ya ushindani uliopo baina ya wanafunzi hawa ambao ni marafik Vifaa vinapatikana kwa wingi kwa shughuli tofauti za michezo kama vile viwanja vya raga na kandanda, sehemu ya kukimbia, viwanja vya mpira wa magongo, uwanja wa kriketi, tenisi na viwanja vya mpira wa kikapu, sehemu za kuogelea, kiwanja cha bogai, sehemu za kukimbia mbio za masafa marefu , mchezo wa "rifle" na uwanja wa mchezo wa gofu. Mashindano baina ya majumba hufanyika kila mara. Kutokana na mashindano haya wawakilishi wa shule huchaguliwa. Daima shule hii huwa na timu zenye ushindani za soka, ukimbiaji, mpira wa kikapu, uogeleaji, mpira wa magongo, karate na voliboli.

Raga ni mchezo uliokatika mila ya shule hii na inasehemu kubwa katika shule hii tangu ilipoanzishwa mwaka wa 1949. Kitambo mchezo huu (pamoja na shule) ulikuwa umehifadhiwa ya wazungu. Tangu wakati huo Lenana imekuwa mmojawapo ya shule nne raga zinazocheza mchezo wa raga wa hali ya juu kwani , [2] Ilihifadhiwa 24 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine. imeweza kushinda mataji mengi, vikombe vingi, na kuwa timu ya shule ya upili pekee kuweza kushinda mashindano katika ngazi ya klabu (tazama Eric Shirley Shield 1977). Lenana huwakilishwa katika mashindano ya raga baina ya shule zingine za upili- Kombe la Prescott, Damu Pevu Shield, mashindano ya taga ya Taifa, sherehe ya raga ya Blackrock na mashindano mengine yote ya wazi. Lenana pia imekuwa mwenyeji wa shindano la raga la wachezaji saba kila upande la ukumbusho wa John Andrews, katika heshima ya mwanafunzi huyo wa zamani. Wanafunzi wengi wa zamani wameweza kuwakilisha nchi ya Kenya kwa kuchezea timu ya taifa katika mashindano ya kimataifa na vilevile kama taaluma yao katika nchi za nje. Timu hiyo inajulikana kama 'Mean Maroon' na huvalia jesi nyekundu lenye waridi nyeupe katika mechi za nyumbani. Mengi kuhusu timu ya raga inapatikana hapa Ilihifadhiwa 24 Aprili 2009 kwenye Wayback Machine..

Mabweni yamekuwa na baadhi ya mabadiliko ya majina kwa sababu ya mwendo wa wakati. Hii ilifanyika ili kutambua nyakati zilizokuwa zinabadilika kutoka wakati wa ukoloni hadi wakati wa uhuru na mashujaa wengi waliohusika katika harakati ya uhuru nchini Kenya, na vilevile mashujaa wengine. Ni dhahiri kuwa mabweni chache bado yanajina yao ya kiasili.
Gabi ya1:

  • Bweni la Kibaki (zamani: Bweni la Thomso n) – lilitajwa baada ya heshima kwa rais wa tatu wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki. Rangi ya bweni hili ni kahawia. Nyumba Michezo ni kahawia.
  • • Bweni la Kinyanjui (zamani: Bweni la Delamar e) – lilitajwa baada ya Chifu Kinyanjui ambaye alikuwa kiongozi wa Kikuyu wakati wa ukoloni. Rangi ya bweni hili ni nyekundu.

Gabi ya 2:

  • Bweni la Mitchell – lilitajwa baada ya gavana wa kikoloni wa Kenya wakati shule ilipoanzishwa, Bwana Philip Euen Mitchell. Rangi ya bweni hili ni manjano.
  • Bweni la Moi (zamani: Bweni la Kirk ) - liltajwa baada ya Rais ya pili ya Kenya aliyestaafuu, Mheshimiwa. Daniel arap Moi. Rangi ya bweni hili ni buluu.

Gabi ya 3:

  • Bweni la Kenyatta (zamani: Bweni la Lugar d) - lilitajwa baada ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kenya, Mzee Jomo Kenyatta. Rangi ya bweni hili ni kijani.
  • Bweni la Ronald Ngala (zamani Bweni la Spek e) – lilitajwa baada ya shujaa wa kabla ya uhuru Ronald Ngala.Rangi ya bweni hili ni zambarau.

Gabi ya4 :

  • Bweni la Boys Francis (zamani: Bweni la Junior Lowe r) - lilitajwa baada mwaanzilishi wa masomo hapa Kenya.Alikuwa mwalimu mkuu katika shule za upili na za kitaifa za Maseno na Alliance (Kenya). Rangi ya bweni hili ni la chungwa.
  • • Bweni la Tom Mboya (zamani: Bweni la Junior Upper ) - lilitajwa baada ya kiongozi wa kisiasa Tom Mboya. Rangi ya bweni hili ni nyeupe na mialamu ya rangi ya nyekundu.

Gabi ya 5:

  • Bweni la James - liltajwa baada ya Mwalimu Mkuu wa kwanza wa shule hiyo, Mheshimiwa RH James. Rangi ya bweni hili ni nyeusi
  • Bweni la Mumia (zamani: Bweni la Grogan) – lilitajwa baada Nabongo Mumia, ambaye alikuwa kiongozi / mfalme wa Waluhya wakati wa ukoloni. Rangi ya bweni hili ni samawati.

Wanafunzi maarufu

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]