Binyavanga Wainaina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Binyavanga Wainaina

Binyavanga Wainaina (alizaliwa mwaka 1971) ni mwandishi wa Kenya.

Alizaliwa Nakuru, nchini Kenya. Alihudhuria masomo ya msingi na sekondari nchini Kenya kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Transkei, Afrika Kusini. Baada ya kumaliza masomo yake alihamia katika jiji la Cape Town ambapo alifanya kazi kama mwandishi wa kujitegemea wa masuala ya chakula na utalii.

Mwezi Julai 2002 Binyavanga alishinda Tuzo ya Caine kwa Uandishi wa Kiafrika. Yeye ndiye mwanzilishi wa jarida la fasihi la Kwani?, ambalo linachukuliwa kuwa ndio gazeti kuu la masuala ya fasihi toka Afrika Mashariki. Hivi sasa anaandika riwaya yake ya kwanza iitwayo The Fallen World of Appearances. Mwaka 2003 alipata tuzo toka Chama cha Wachapishaji wa Kenya (Kenya Publishers Association) kutokana na juhudi zake za kuendelea fasihi ya Kenya.

Hivi sasa anasoma shahada ya pili ya Uandishi wa Ubunifu katika Chuo Kikuu cha East Anglia. Kazi zake zimetoka katika magazeti na majarida mbalimbali kama vile National Geographic, The East African, The Sunday Times (ya Afrika Kusini), The Guardian (ya Uingereza).

Baadhi ya kazi alizoandika ni:

  • Discovering Home (Hadithi fupi, G21Net, 2001)
  • An Affair to Dismember (Hadithi fupi)
  • Beyond the River Yei: Life in the Land Where Sleeping is a Disease (Riwaya ya picha pamoja na Steven Torfinn, Kwani Trust).

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]