KCSE

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search


KCSE, kwa kimombo, Kenya Certificate of Secondary Education, ni shahada ambayo huchukuliwa baada ya mtu kukamilisha elimu ya sekondari.

Mtihani wa kwanza ulifanyika mwaka wa 1989 wakati uo huo ukiwa mwisho wa Kenya Advanced Certificate of Education (KACE), ikiwa ni mahitaji ya wastani ya yeyote atakayetaja kujiunga na vyuo vikuu vya Kenya. Awali, KCSE ilikuwa ikitahini masomo kumi. Tangu hapo, KCSE imesahihishwa na wataalam mara mbili, na idadi ya masomo ikawa saba.

Mtihani hufanywa wakati wa Oktoba na Novemba na matokeo hutolewa mwezi wa Februari mwaka unaofuata.

Masomo ya lazima Kundi la pili Kundi la tatu Kundi la nne Kundi la tano
Kiingereza, Kiswahili, Hisabati Biolojia, Fizikia, Kemia na Sayansi za Biolojia (zinazofanywa na watahiniwa vipofu) Historia na Somo la Serikali, Jiografia, Somo la Dini ya Kikristo, Somo la Dini ya Kiislamu na Somo la Dini ya Kibaniani Sayansi Kimo ,Usanii na Uundaji, Kilimo, Masomo ya Tarakilishi, Masomo ya ndege Kifaransa, Kijerumani, Kiarabu, Muziki, Masomo ya Biashara

Ili kupeana alama, watahiniwa lazima wafanye masomo ya lazima tatu, angalau sayansi mbili, moja ya kundi la tatu na angalau moja yenye kufanya uchunguzi au ya kiufundi(kundi la nne) (tazama jedwali hapo juu).

Mitihani wa KCSE hufanywa chini ya usimamizi wa hali ya juu ili kuepukana na vitendo vya udanganyifu na hudumu kwa muda wa mwezi mmoja. Kuna adhabu kali kwa visa vya udanganyifu kutoka Baraza la Mitihani ya Kitaifa ya Kenya na matokeo ya wanafunzi wanaoshikwa hutupiliwa mbali. Kwa kawaida, mtihani huanza 22 Oktoba na kumalizika mwishoni mwa Novemba. Kuanzia Desemba, mtihani husahihishwa na matokeo kutolewa 26 Februari mwaka unaofuata. Matokeo ya mitihani hutangaziwa umma na Waziri wa Elimu na wanafunzi na shule mia moja bora hufunuliwa vyombo vya habari siku iyo hiyo ya kutangaza. Upangaji wa shule bora hugawanywa katika shule binafsi, shule za umma na za mikoa. Kila kundi likiwa na shule mia moja bora.

Alama za mtihani ni kama ifuatavyo:

 • A (80% na zaidi yake)
 • A- (79-75)
 • B + (70-74)
 • B (65-69)
 • B- (60-65)
 • C + (55-59)
 • C (50-54)
 • C- (45-49)
 • D + (40-44)
 • D (35-39)
 • D- (30-34)
 • E (0-29)

Nchini Kenya, mtihani huu ndio kiiingilio katika vyuo vikuu vya umma na vya kibinafsi na alama ya chini sana huwa ni C+(cha chanya). Wanafunzi wapatao alama chini ya C+ hujiunga na taasisi nyingine za msingi kwa mafunzo yasiyo ya digri. Kwa muda uliopita, serikali imechukua hatua kadha wa kadha ili kuhakikisha na kudumisha uaminifu katika ufanyizi wa mtihani wa KCSE. Hata hivyo, kumekuwa na matukio ya ukiukaji wa hatua hizi na visa vya wizi wa mtihani kwa baadhi ya wanafunzi ambao hupita sana kama hawagunduliwa. Visa hivi vinapogunduliwa,wanafunzi hawa huadhibiwa kwa kutupilia mbali matokeo yao ya mitihani na maafisa walioshiriki pia kushtakiwa katika mahakama ya sheria.

Kila mwaka, mamia ya maelfu ya wanafunzi hufanya mtihani huu baada ya miaka minne ya kuwa katika shule ya sekondari na kumaliza kosi hii. Pia, huu mtihani ndio huamuwa maisha yajao ya mtu binafsi. Alama nzuri ni ishara ya kuwa mtahiniwa hana budi kupata nafasi nzuri katika chuo kikuu cha umma au binafsi nchini.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]