Shota Rustaveli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shota Rustaveli - picha kwenye ukuta wa kanisa alikozikwa

Shota Rustaveli (1172 - 1216) alikuwa mshairi nchini Georgia wakati wa karne ya 12. Hutazamwa kama mwanzilishi wa fasihi ya Kigeorgia isiyo ya kidini.

Utenzi wake unaojulikana zaidi ni "Shujaa anayevaa ngozi ya chui"; ni utenzi wenye beti 1,550 uliosimuliwa tangu siku za mshairi mwenyewe na Wageorgia wakiwa na sherehe au sikukuu.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Hakuna uhakika juu ya maisha yake lakini habari za kale kutoka Georgia zasema kwamba alipata elimu nzuri nchini Georgia na baadaye Ugiriki yaani katika Milki ya Bizanti. Anaaminiwa alikuwa waziri wa malkia wa Georgia hata mpenzi wake alipaswa kuondoka nchini wakati malkia alipoolewa akahamia Yerusalemu. Huko alijitolea kupamba na kutengeneza monasteri ya Msalaba Mtakatifu mjini Yerusalemu alikozikwa. Uchoraji wa ukutani unamkumbuka hadi leo.

Kazi yake[hariri | hariri chanzo]

Ukurasa wa utenzi wake

"Shujaa anayevaa ngozi ya chui" imetafsiriwa katika lugha nyingi. Ilichapishwa mara ya kwanza mjini Tbilisi mwaka 1712.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shota Rustaveli kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.