Sheri-Ann Brooks
Sheri-Ann Brooks (alizaliwa 11 Februari 1983 katika mji wa Kingston) ni mwanariadha wa Jamaika ambaye ni mtaalamu katika mbio ya mita 100.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Brooks aliwakilisha nchi ya Jamaika katika Olimpiki ya 2008 mjini Beijing. Akiwa pamoja na Shelly-Ann Fraser, Aleen Bailey and Veronica Campbell-Brown walishiriki katika mbio za 4 x 100m. Katika mzunguko wa kwanza , Jamaika ilishinda nchi zaUrusi, Ujerumani na Uchina. Muda wa Jamaika wa sekunde 42.24 ulikuwa wa kwanza katika mataifa 16 yaliyoshiriki katika mbio hiyo. Kutokana na matokeo hayo, Jamaika walihitimu kushiriki katika fainali, Brooks na Bailey wakibadilishwa na Sherone Simpson na Kerron Stewart. Jamaika hawakumaliza mbio hiyo kutokana na kosa la kubadilisha nafasi kati ya wanariadha wawili. [10]
Alihitimu kushindana katika mbio ya 100m katika Shindano la Dunia la Riadha la 2009 alipokuwa #3 katika mashindano ya kitaifa ya Jamaica akiwafuata Fraser na Stewart.
Mnamo mwezi Juni 2009, Brooks alikuwa mmoja wa wanariadha watano wa timu ya Jamaika walioripotiwa kuwa sampuli ya mikojo yao ilionyesha ishara za kuwa na kemikali zilizopigwa marufuku. Brooks aliachiliwa kuendelea kushiriki katika riadha kwa kuwa Tume dhidi ya Utumiaji wa Dawa Haramu nchini Jamaika ilikuwa imefanya majaribio ya kisayansi kwa sampuli yake bila Brooks kujua. Hata hivyo, Muungano wa Riadha ya Jamaika ilimtoa kutoka mbio za 4 x 100 katika Mashindano ya Mabingwa kama tahadhari.
Mafanikio
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Shindano | Pahali pa kushindana | Matokeo | Aina ya mbio |
---|---|---|---|---|
2006 | Michezo ya Jumuia ya Madola | Melbourne, Australia | 1 | 100 m |
5 | 200 m | |||
1 | 4 x 100 m | |||
2007 | Shindano la Pan Amerika | Rio, Brazil | 2 | 200 m |
1 | 4 x 400 m | |||
Shindano la Mabingwa Duniani 2007 | Osaka, Japan | 2 | 4 x 100 m |
Muda bora za kibinafsi
[hariri | hariri chanzo]- 100 mita - 11.05 s (2007)
- 200 mita - 22.78 s (2007)
- 400 mita - 53.95 s (2006)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Athlete biography: Sheri-Ann Brooks, beijing2008.cn,
- Foster, Anthony (2009-06-28). Bolt 9.86 and Fraser 10.88; Walker and Phillips excel over hurdles - JAM Champs , . IAAF.
- "Sherri Ann Brooks cleared to run for Jamaica". The Guardian (The Guardian).
- IAAF wait for Jamaica drug ruling . BBC Sport (2009-08-11).
- Jamaican five withdrawn by team . BBC Sport (2009-08-19).
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- IAAF wasifu wa Sheri-Ann Brooks