Sewa Haji Paroo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Sewa Haji)

'

Sewa Haji Paroo
Sewa Haji
Amezaliwa1851
Amefariki10 Februari 1897
Kazi yakemfanyabiashara


Sewa Haji Paroo (Bagamoyo, 1851 - mjini Zanzibar, 10 Februari 1897) alikuwa mfanyabiashara mwenye asili ya Uhindi. Alimfanyia biashara Sultani wa Zanzibar. Huko Bagamoyo alifadhili ujenzi wa shule na hospitali. Pia alianzisha ujenzi wa Hospitali ya Sewa Haji mjini Dar es Salaam[1] iliyoendelea na kuwa hospitali ya Muhimbili[2].

Sewa Haji huangaliwa kama mfadhili mkuu katika Afrika Mashariki, k.mf. alichangia ujenzi wa shule, msikiti na visima mbalimbali mjini Bagamoyo. Pia aliifadhili safari ya Henry Morton Stanley.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. [https://ismailimail.blog/2015/01/26/muhimbili-and-bagamoyo-hospitals-mwambao-school-the-legacy-of-sewa-haji-paroo-in-tanzania/ Muhimbili and Bagamoyo Hospitals, Mwambao School: The legacy of Sewa Haji Paroo in Tanzania], ismailimail.blog 26.01.2015, iliangaliwa Februari 2015
  2. About MNH, tovuti ya Muhimbili National Hospital, iliangaliwa Februari 2021
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sewa Haji Paroo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.