Nenda kwa yaliyomo

Bocho (Scorpaeniformes)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Setarchidae)
Bocho
Bocho au mbevu mwekundu (Scorpaena scrofa)
Bocho au mbevu mwekundu (Scorpaena scrofa)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Scorpaeniformes (Samaki kama mabocho)
Nusuoda: Scorpaenoidei (Mabocho)
Ngazi za chini

Familia 14 na spishi >1000, 48 katika Afrika ya Mashariki:

Mabocho ni spishi za samaki za familia 15 za nusuoda Scorpaenoidei katika oda Scorpaeniformes zinazopatikana katika bahari zote za dunia na pengine katika maji baridi. Spishi za familia Plectrogeniidae na Triglidae huitwa mnuvi kama spishi za nusuoda Platycephaloidei. Mabocho hawa sio samaki washawishi kama samaki wa oda Lophiiformes waitwao mabocho pia.

Mabocho wengi wanaishi kwenye sakafu ya bahari kwa vina vya m makumi hadi mamia na hata mpaka zaidi m 3000. Spishi hizi hukaa kwa kawaida katikati ya miamba ambapo zinangoja mpaka mbuawa anakuja karibu kisha kummeza haraka sana. Huitwa mbevu, shinda-dovu au mbera pia. Spishi nyingine huogelea polepole na kuvamia mbuawa. Hizi huitwa chale, kisheshe au mchafe kwa kawaida.

Mabocho ni wagwizi ambao hujilisha hususan kwa gegereka na samaki wadogo. Spishi nyingi huishi kwenye sakafu ya bahari katika maji kame, ingawa spishi kadhaa hujulikana kutoka maji ya kina kikubwa na kadirifu na hata kutoka kwenye maji baridi. Kwa kawaida huwa na kichwa chenye miiba na mapeziubavu na pezimkia yaliyoviringana. Takriban spishi zote zina urefu wa chini ya sm 30, lakini ukubwa kamili wa oda hutofautiana kutoka samaki-mahameli, ambao wanaweza kuwa na urefu wa sm 2 tu wakiwa wapevu, mpaka mnuvi-tondi, ambaye anaweza kufikia urefu wa sm 150.

Spishi za Afrika ya Mashariki

[hariri | hariri chanzo]
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bocho (Scorpaeniformes) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.