Bocho (Lophiiformes)
Bocho | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Bocho mwekundu (Antennatus coccineus)
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Nusuoda 5 na familia 18:
|
Mabocho ni spishi za samaki washawishi wa baharini wa oda Lophiiformes wanaopatikana katika bahari zote. Samaki hawa wanaishi kwenye sakafu ya bahari kwa kina cha m 40 hadi zaidi ya m 3,000. Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki zinaitwa chura-bahari, guguye au shinda-dovu pia. Kuna spishi nyingine katika oda Scorpaeniformes zinazoitwa bocho au shinda-dovu pia, kwa sababu zinafanana na spishi za Lophiiformes.
Hawa ni samaki wenye mifupa wanaoshawishi mbuawa kwa chambo ambako ni ukuaji wa nyama kwenye ncha ya mwiba au uzi juu ya kichwa cha samaki (eska na ilisio). Mara nyingi eska hutoa mwanga, katika bahari za kina kikubwa hasa.
Baadhi ya mabocho pia hujulikana kwa tofauti kubwa sana kati ya jinsia na ufaano wa kijinsia wa dume mdogo na jike mkubwa zaidi mno, kinachoonekana katika nusuoda Ceratioidei. Katika spishi hizi, madume wanaweza kuwa wadogo kuliko majike kwa taratibu kadhaa na hata kuishi kama kidusia juu ya majike.
Mabocho hutokea duniani kote. Wengine ni wa pelajiki (wanaoishi mbali na sakafu ya bahari), huku wengine ni wa bentiki (wanaoishi karibu na au kwenye sakafu ya bahari). Wengine wanaishi bahari ya kina kikubwa (k.m. Ceratiidae) na wengine kwenye tako la bara (k.m. spishi za Antennariidae na Lophiidae). Spishi nyingi za kipelajiki ni bapa kimbavuni, lakini spishi za kibentiki ni bapa sana juu-chini mara nyingi wenye domo pana lililoelekezwa juu.
Spishi za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]- Antennarius hispidus, Bocho Njano (Shaggy frogfish)
- Antennarius indicus, Bocho Hindi (Indian frogfish)
- Antennarius maculatus, Bocho Sugu (Warty frogfish)
- Antennarius striatus, Bocho Milia (Striated frogfish)
- Antennatus coccineus, Bocho Mwekundu (Scarlet frogfish)
- Antennatus dorehensis, Bocho Kijivu (New Guinean frogfish)
- Antennatus nummifer, Bocho Pezi-doa (Spotfin frogfish)
- Chaunax heemstraorum, Chura-bahari wa Heemstra (Heemstra's frogmouth)
- Chaunax hollemani, Chura-bahari wa Holleman (Holleman's frogmouth)
- Chaunax penicillatus, Chura-bahari Kalamu (Pencil coffinfish)
- Halieutopsis galatea, Bocho-raketi (Pale seabat)
- Lophiodes mutilus, Guguye Laini au Shinda-dovu (Smooth angler)
- Lophiomus setigerus, Guguye Domo-jeusi au Shinda-dovu (Blackmouth angler)
- Malthopsis bradburyae, Bocho-raketi Pembetatu (Bradbury's triangular batfish)
- Melanocetus johnsonii, Guguye Kibyongo (Humpback anglerfish)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Bocho njano
-
Bocho sugu
-
Bocho milia
-
Guguye domo-jeusi
-
Guguye kibyongo
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
- Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Mabocho kwenye hifadhidata ya samaki Ilihifadhiwa 11 Februari 2019 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bocho (Lophiiformes) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |