Nenda kwa yaliyomo

Serbia na Montenegro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Serbia na Montenegro

Serbia na Montenegro (Kiserbia Србија и Црна Гора / Srbija i Crna Gora) ilikuwa nchi ya Ulaya kwenye rasi ya Balkani kati ya 2003 hadi 2006.

Ilikuwa aina ya shirikisho la madola ya Serbia na Montenegro. Shirikisho hili lilikuwa yote yaliyobaki ya Yugoslavia ya awali. Serbia na Montenegro ziliwahi kuwa jamhuri za Yugoslavia zikabaki baada ya kuondoka kwa jamhuri zote nyingine kama vile Kroatia, Slovenia, Masedonia na Bosnia-Herzegovina hadi mwaka 1992.

Tangu 1992 Serbia na Montenego ziliendela kushikamana kwa jina la Shirikisho la Jamhuri ya Yugoslavia. Mwaka 2003 zilipatana kuunda jumuiya mpya ya madola yao kwa jina la "Serbia na Montenegro" iliyokuwa ushirikiano wa nchi mbili zilizojitegemea.

Kila nchi ilikuwa na pesa yake.

Mwaka 2006 wananchi wa Montenegro walipiga kura kuondoka katika umoja huu na kuwa nchi ya pekee kabisa.