Nenda kwa yaliyomo

Seli nyeupe za damu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Seli nyeupe)
Seli nyeupe na nyinginezo zinavyoonekana kwa hadubini.

Seli nyeupe za damu (kwa Kiingereza: White blood cells, kifupi: WBCs; pia leukocytes au leucocytes) ni miongoni mwa aina za seli za damu. Ndizo seli zinazohusika na mfumo wa kingamaradhi ili kulinda mwili hidi ya maambukizi.

Kuna aina tatu za seli za damu, ambazo ni seli nyekundu, seli sahani pamoja na seli nyeupe. Kwa idadi seli nyeupe ndizo zilizo chache kuliko seli nyingine zote.

Zinapatikana katika mwili wote.[1]

Seli nyeupe hufanya kazi ya kupambana na viini vya magonjwa mbalimbali. Viini vya magonjwa huweza kuwa vijidudu, bakteria au virusi. Seli nyeupe hufanya kama askari wa mwili. Viini vya magonjwa vinapoiingia mwilini huanza kushambulia kwanza seli nyeupe za damu. Hivyo kama seli hizo ni dhaifu basi ni rahisi mwili kushambuliwa na viini hvyo.

Seli nyeupe huimarishwa kwa kula mlo kamili hasa vyakula venye vitamini. Vyakula vyenye vitamini ni kama matunda na mbogamboga hasa za majani. Seli nyeupe huimarishwa kwa vitamini kwani magonjwa mengi husababishwa na upungufu wa vitamini.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Maton, D., Hopkins, J., McLaughlin, Ch. W., Johnson, S., Warner, M. Q., LaHart, D., & Wright, J. D., Deep V. Kulkarni (1997). Human Biology and Health. Englewood Cliffs, New Jersey, US: Prentice Hall. ISBN 0-13-981176-1.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Seli nyeupe za damu kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.