Nenda kwa yaliyomo

Milima ya Sayan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Sayan Mountains)
Ziwa la "Mapepo ya milima"
Sayan Magharibi

Milima ya Sayan ni safu ya milima kusini mwa Siberia, Urusi, hasa kwenye Jamhuri ya Tuva, na kaskazini mwa Mongolia . Hapo zamani milima ilikuwa mpaka kati ya Mongolia na Urusi. [1]

Vilele vya Milima ya Sayan na maziwa baridi kati yake ni chanzo cha matawimito yanayounda mto Yenisei, unaoanza hapa na kuendelea kwa zaidi ya kilomita 3000 hadi Bahari ya Aktiki. Hili ni eneo lililotengwa kwa miaka mingi, kwa kuwa limefungwa na Umoja wa Kisovyeti tangu mwaka 1944. [2]

Mlima Mönkh Saridag.

Sayan Mashariki inaenea kwa km 1,000 kutoka mto Yenisei hadi Ziwa Baikal. Sayan Magharibi inaendeleza Milima ya Altai, ikienea kwa km 500 kutoka longitudo ya 89° hadi katikati ya Mashariki.

Wakati mwinuko wa wastani ni mita 2,000 hadi 2,700, vilele vya miamba migumu kama itale hufikia zaidi ya mita 3,000. Kilele cha juu kabisa ni Mönkh Saridag chenye kimo cha mita 3,492.

Vidokezo

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Sayan Mountains". Iliwekwa mnamo 2006-12-25.
  2. "Tuva and Sayan Mountains". Geographic Bureau - Siberia and Pacific. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-11-26. Iliwekwa mnamo 2006-10-26.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Milima ya Sayan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.