Nenda kwa yaliyomo

Mhozo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Saxicola)
Mhozo
Mhozo utosi-mweupe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Muscicapoidea (Ndege kama shore)
Familia: Muscicapidae (Ndege walio na mnasaba na shore)
J. Fleming, 1822
Nusufamilia: Saxicolinae (Ndege walio na mnasaba na mihozo)
Vigors, 1802
Ngazi za chini

Jenasi 3:

Mihozo ni ndege wa jenasi Oenanthe, Saxicola na Campicoloides. Zamani wataalamu waliwaweka katika familia ya mikesha (Turdidae), lakini siku hizi mihozo huainiwa baina ya shore (Muscicapidae). Mihozo wana mabaka maalum meusi na meupe au mekundu na meupe kwa kiuno na mkia wao mrefu. Ndume ni maridadi kuliko jike. Hukaa chini na hula wadudu. Wanatokea nyanda kavu katika Afrika, Ulaya na Asia. Spishi zinazozaa katika nchi za kaskazini huhamia Afrika wakati wa baridi. Hujenga matago yao ndani ya mianya ya miamba au vishimo visivyotumika.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine

[hariri | hariri chanzo]