Sasini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Nembo ya Kampuni ya Sasini

Sasini ni mojawapo wa wazalishaji wakubwa wa chai na kahawa, pia ni mojawapo wa "Wakubwa Sita" wa kuzalisha chai.

Makao makuu ya kampuni hii yamo mji wa Nairobi na kampuni hii imeorodheshwa katika Soko la Hisa la Nairobi.

Sasini ni moja ya kampuni za Kundi la Sameer, kundi hili pia lina makao yake Kenya.

Operesheni[hariri | hariri chanzo]

Chai[hariri | hariri chanzo]

Mojawapo ya bidhaa za Sasini:Sasini Chai

Chai inapandwa na shirika dogo la Sasini,liitwalo Kipkebe.Kipkebe linaendesha viwanda viwili vya CTC(Kipkebe na Keritor) vyenye vinahudumia mashamba manne yaliyo magharibi wa Kenya. Vikiwa pamoja,vinaweza kuzalisha zaidi ya kilogramu milioni 8.5 kila mwaka.Chai hii inauzwa na Sasini kwa nchi kama Misri,Uingereza na nchi nyinginezo.

Kahawa[hariri | hariri chanzo]

Kahawa Mashamba ya kampuni hii yako katika Mkoa wa Kati nchini Kenya wakiwa na vituo vyao Wilaya ya Kiambu na Wilaya ya Nyeri.Shamba lao la Mweiga katika Wilaya ya Nyeri lina uwanja wa ndege wa kusaidia katika usafirishaji ya shehena ya ndege isiyokuwa chini ya mifuko 5,700 ya kahawa.Vifaa vya Sasini vimewafanya wasaidike sana kwa muda ambao kumekuwa na migogora katika usimamizi wa Muungano wa Wapanzi wa Kahawa.Hivyo basi,Sasini ikapata faida kwa muda wa shida hizi za umeneja.

Maziwa na Mimea ya Kuuza Ng'ambo[hariri | hariri chanzo]

Maziwa na Mimea ya Kuuza Ng'ambo:Sekta ya maziwa ya Sasini inazalisha maziwa na maziwa mala yenye mionjo tofauti,bidhaa hizi huuzwa katika soko lolote kwa jumla.Sekta yake ya mmea ya kuuzwa ng'ambo inanawiri,huku wakipanda mahindi na mboga mengineo.

Maduka ya kuuza kahawa[hariri | hariri chanzo]

Sasini,hivi majuzi,imeanza kufunugua maduka ya kuuza kahawa mjini Nairobi, ikiwa na lengo la kufanya upanuzi wa biashara yao hadi nje ya Kenya.Hii inaonekana kama kuongeza thamani kwa hisa zao.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sasini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.