Sangari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sangari
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja)
(bila tabaka): Commelinids (Mimea kama jaja)
Oda: Poales (Mimea kama manyasi)
Familia: Poaceae (Manyasi)
Nusufamilia: Panicoideae
Jenasi: Digitaria
Spishi: D. abyssinica
(Hochst.. ex. A.Rich.) Stapf

Sangari (Digitaria abyssinica) au kidiru ni spishi ya nyasi katika nusufamilia Panicoideae iliyo na mnasaba na mfonio (D. Exilis na D. Iburua). Inafanana pia na lugowi (Cynodon sp.) lakini masuke yake ni membamba zaidi. Asili ya spishi hii ni Afrika ya Mashariki na ya Kati lakini imewasilishwa katika Afrika ya Kusini, Afrika ya Magharibi na Asia. Nyasi hili ni gugu baya katika mashamba.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]