Sami Khedira

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sami Khedira akikimbiza mpira.

Sami Khedira (alizaliwa 4 Aprili 1987) ni mchezaji wa soka wa Ujerumani ambaye anacheza kama kiungo wa kati katika timu ya Italia Juventus na timu ya taifa ya Ujerumani.

Khedira alianza kazi yake katika timu ya VfB Stuttgart na kushinda Bundesliga mwaka 2007, kabla ya kuhamia Real Madrid mwaka 2010. Katika misimu yake mitano nchini Hispania, alishinda mataji saba ya ndani na kimataifa, ikiwa ni pamoja na Ligi ya Mabingwa ya Ulaya (UEFA) mwaka 2014.

Mwaka 2015, alihamia Juventus iliyopo Italia kwa uhamisho wa bure, na mara moja alishinda cheo cha Serie A katika msimu wake wa kwanza na klabu hiyo.

VfB Stuttgart[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya kujiunga na timu ya vijana wa VfB Stuttgart mwaka 1995, alichezea Oeffingen. Katika miezi ya kwanza ya msimu wa 2006-07, aliitwa kwenye kundi la Bundesliga VfB na meneja Armin Veh.Alisaini mkataba wa miaka mitatu na VfB.

Sami Khedira akiwa mazoezini

Real Madrid[hariri | hariri chanzo]

Mnamo tarehe 30 Julai 2010, Khedira alihamia Real Madrid kwa ada isiyojulikana na kusaini mkataba hadi 2015. Khedira alicheza mechi yake ya kwanza mnamo tarehe 13 Agosti katika mechi ya kirafiki dhidi ya Bayern Munich, ambapo Real Madrid ilishinda 4-2 kwa Penati.

Juventus[hariri | hariri chanzo]

Mnamo tarehe 9 Juni 2015, upande wa Italia Juventus alitangaza kwamba Khedira amesaini mkataba wa miaka minne kwa uhamisho wa bure. Hatua hiyo ilikamilishwa tarehe 1 Julai mwanzoni mwa msimu wa 2015-16,Khedira imeipatia mafanikio makubwa sana Juventus.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sami Khedira kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.