Sadoth na wenzake

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sadoth na wenzake 128 (karibu wote walifariki Seleucia, leo nchini Iraq, 342) walikuwa Wakristo, wakiwemo hasa wakleri na watawa, waliouawa kikatili na Wasasanidi kwa sababu walikataa kuabudu jua kutokana na imani yao baada ya kuteswa gerezani miezi mitano.

Sadoth alikuwa askofu mkuu wao tangu mwaka mmoja tu. Hatimaye alitengwa nao na kupelekwa Beth Lapat kukatwa kichwa huko[1].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 18 Februari[2] au 20 Februari.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • (Kilatini) Abbeloos, J. B., and Lamy, T. J., Bar Hebraeus, Chronicon Ecclesiasticum (3 vols, Paris, 1877)
  • (Kilatini) Assemani, J. A., De Catholicis seu Patriarchis Chaldaeorum et Nestorianorum (Rome, 1775)
  • (Kilatini) Brooks, E. W., Eliae Metropolitae Nisibeni Opus Chronologicum (Rome, 1910)
  • (Kilatini) Gismondi, H., Maris, Amri, et Salibae: De Patriarchis Nestorianorum Commentaria I: Amri et Salibae Textus (Rome, 1896)
  • (Kilatini) Gismondi, H., Maris, Amri, et Salibae: De Patriarchis Nestorianorum Commentaria II: Maris textus arabicus et versio Latina (Rome, 1899)
  • (Kifaransa) Jérôme Labourt, Le christianisme dans l'empire perse sous la dynastie Sassanide (224-632), Paris, 1904, p. 72
  • (Kilatini) Michel Le Quien, Oriens christianus in quatuor Patriarchatus digestus, Parigi, 1740, Tomo II, coll. 1108-1109 (n. X)
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.