Nenda kwa yaliyomo

Rudolf Clausius

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rudolf Julius Emanuel Clausius.

Rudolf Julius Emanuel Clausius (2 Januari 1822 - 24 Agosti 1888) alikuwa mwanafizikia na mwanahisabati wa Ujerumani, mwanzilishi wa sayansi ya themodanamikia.

Kwa kurekebisha kauli ya Sadi Carnot, ijulikanayo kama mzunguko wa Carnot, alitoa ukweli kuhusu nadharia ya joto na msingi wa sauti. Lengo lake katika msukumo wa nguvu ya joto 1850, alianzisha msingi wa wazo la sheria ya pili ya themodanamikia. Mwaka 1865 aliingiza dhana ya entropy. Mwaka 1870 alianzisha nadharia ya virial ambayo ilitumika kwenye joto.

Rudolf Julius Emanuel Clausius alizaliwa Köslin (kwa sasa Koszalin, mji wa Polandi) katika ngome ya wilaya ya Pomerania nchini Prussia.

Baba yake kiongozi wa kanisa na msimamizi wa shule na Rudolf alisoma kwenye shule ya baba yake (Julius Emanuel Clausius).

Baada ya miaka kadhaa alienda Gymnasium Stettin (kwa sasa Szczecin). Alimaliza elimu ya juu katika chuo kikuu cha Berlin (University of Berlin) na kufanikiwa kuchukua masomo ya Hisabati na Fizikia akiwa na wengine kama Gustav Magnus, Peter Gustav Lejeune Dirichlet na Jakob Steiner mnamo mwaka 1844. Pia alisoma historia na Leopold von Ranke.

Mnamo mwaka 1847, alifanikiwa kuchukua uzamivu katika chuo kikuu cha Halle, kitivo cha Madhara ya anga.

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rudolf Clausius kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.