Rijili ya Jabari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Rijili ya Jabar)
Mahali pa Rijili Jabari (=Rigel) katika Jabari - Orion
Ulinganifu wa ukubwa baina ya Rijili Jabari na Jua letu (kushoto)

Rijili ya Jabari (en:Rigel) ni nyota jitu katika kundinyota la Jabari (en:Orion).

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jina la Kiswahili Rijili ya Jabari linatokana na ar. رجل الجبار rijil-al-jabar. Maana ya jina ni "mguu wa jitu" maana mataifa ya kale waliona kundinyota lote kama picha ya jitu katika anga. Jina la kimagharibi "Rigel"[1] linatokana pia na neno lilelile la Kiarabu kwa "mguu" yaani رجل inayoandikwa kwa herufi za Kilatini ama "rijil" au "rigil". [2].

Jina la kitaalamu kufuatana na mfumo wa Bayer ni Beta Orionis kwa maana ya kwamba ilitazamiwa kuwa nyota ya pili kwa uangavu kati ya nyota za Jabari (Orion).

Tabia[hariri | hariri chanzo]

Rijili Jabari inaonekana kama nyota angavu sana kwenye anga la usiku. Mwangaza unaoonekana ni 0.13 mag kwa hiyo ni nyota angavu ya saba angani. Rangi yake ni nyeupe hadi buluu-nyeupe. Katika darubini kubwa inaonekana kama nyota maradufu yaani mfumo wa nyota tatu, labda pia tano.

Umbali na dunia ni miaka nuru 778.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. ni pia jina lililokubaliwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia, ling. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union, iliangaliwa Julai 2017
  2. Herufi ya ج kwa kawaida husomwa kama "j" jinsi ilivyo pia kwenye Rasi ya Uarabuni lakini pale Misri matamshi ya "g" ni kawaida. Vokali fupi za i na e hazitofautishwi katika mwandiko wa Kiarabu