Rijili ya Jabari
Rijili ya Jabari (en:Rigel) ni nyota jitu katika kundinyota la Jabari (en:Orion).
Jina
[hariri | hariri chanzo]Jina la Kiswahili Rijili ya Jabari linatokana na ar. رجل الجبار rijil-al-jabar. Maana ya jina ni "mguu wa jitu" maana mataifa ya kale waliona kundinyota lote kama picha ya jitu katika anga. Jina la kimagharibi "Rigel"[1] linatokana pia na neno lilelile la Kiarabu kwa "mguu" yaani رجل inayoandikwa kwa herufi za Kilatini ama "rijil" au "rigil". [2].
Jina la kitaalamu kufuatana na mfumo wa Bayer ni Beta Orionis kwa maana ya kwamba ilitazamiwa kuwa nyota ya pili kwa uangavu kati ya nyota za Jabari (Orion).
Tabia
[hariri | hariri chanzo]Rijili Jabari inaonekana kama nyota angavu sana kwenye anga la usiku. Mwangaza unaoonekana ni 0.13 mag kwa hiyo ni nyota angavu ya saba angani. Rangi yake ni nyeupe hadi buluu-nyeupe. Katika darubini kubwa inaonekana kama nyota maradufu yaani mfumo wa nyota tatu, labda pia tano.
Umbali na dunia ni miaka nuru 778.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ ni pia jina lililokubaliwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia, ling. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union, iliangaliwa Julai 2017
- ↑ Herufi ya ج kwa kawaida husomwa kama "j" jinsi ilivyo pia kwenye Rasi ya Uarabuni lakini pale Misri matamshi ya "g" ni kawaida. Vokali fupi za i na e hazitofautishwi katika mwandiko wa Kiarabu