Nenda kwa yaliyomo

Rich Msafii

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Makala hii inahusu mada au mtu asiyejulikana sana. Kuna mashaka kama mada inastahili kuwa na makala katika kamusi. Onyo hili linaweza kuwekwa pia kama makala haionyeshi umaarufu, hata kama upo.

Watumiaji wanaombwa kushiriki katika majadiliano kama makala hii inafaa kubaki au la. Tazama:Wikipedia:Umaarufu

Unaweza kuondoa kigezo hiki kama majadiliano yametokea na washiriki walipatana.

Richard Richard Nyondo (maarufu kama Rich Msafii, alizaliwa mkoa wa Iringa) ni mtangazaji wa Tanzania ambaye anatangaza kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa East Africa Radio.

Rich Msafii pia ni mtangazaji wa kipindi cha Bongo Fleva Top 20 kinachorushwa East Africa Radio kila Jumamosi lakini pia alikuwa ni ripota wa kipindi cha EATV cha kuitwa E- Newz.[1]

Rich Msafii ameshafanya mahojiano na watu mbalimbali mashuhuri ikiwemo Mbosso, Harmonize, Marioo, Darassa, Mwana FA, Joseph Kusaga, Ruger na Krizbeatz kutokea Nigeria.[2]

Maisha Ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

Rich Msafii alizaliwa Iringa na baadaye yeye pamoja na famiia yake wakahamia mkoa wa Dar es Salaam, ambako ndiko alipoanzisha safari yake katika tasnia ya utangazaji.

Rich alipata elimu yake ya sekondari ya St Michaels na baadae alihamia kwenye shule ya Sekondari ya Imagevosa ambapo alimalizia elimu yake ya sekondari.

Mwaka 2020 Rich aliingia rasmi East Africa Radio akiwa kama ripota wa kipindi cha E-NEWS na baadae alipata nafasi ya kuwa mtangazaji mwenza kwenye kipindi cha Planet Bongo.[3]

Mwaka 2024, Rich Msafii alitangazwa kama mtangazaji mkuu wa Planet Bongo mara baada ya Dullah Planet na Lesa Sid kuondoka.[4] [5]

Watu Waliomshawishi

[hariri | hariri chanzo]

Kupitia mahojiano mbalimbali aliyoyafanya, Rich Msafii mtangazaji wa zamani wa Planet Bongo, Salama Jabir na B Dozen wa Clouds FM kama moja ya watangazaji waliomshawishi kuingia kwenye utangazaji.[6]

Mwaka 2023, Rich Msafii kupitia kipindi cha Planet Bongo, alitajwa kuwania tuzo za Unkut Hip Hop Awards kutokea nchini Kenya ambapo alitajwa kuwania kipengele cha Best Hip Hop Radio Show.[7]

  1. "Biography: The story of Rich Msafii and how he is changing the Tanzania's media scene". Latest East African & Bongo Flava Music, Songs & Video - Notjustok (kwa American English). 2024-09-10. Iliwekwa mnamo 2024-09-12.
  2. EastAfricaTV (2022-09-28), Ruger atoa tamko baada ya kutua bongo | Sababu ya kuziba jicho lake | kufanya balaa Oktoba 1, iliwekwa mnamo 2024-09-12
  3. TRANSSION: LHX. "Boomplay Music". Boomplay Music - WebPlayer (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-09-12.
  4. "Lesa wa Planet Bongo aondoka East Africa Radio". TanzaniaWeb. 2024-04-15. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-09-12. Iliwekwa mnamo 2024-09-12.
  5. Editor (2024-04-13). "Mtangazaji wa Planet Bongo, Lesa aondoka East Africa Radio". JamboMail.com - Burudani, Makala, Michezo, New Music, Mambo 10 & Lifestyle (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2024-09-12. {{cite web}}: |author= has generic name (help)
  6. "Biography: The story of Rich Msafii and how he is changing the Tanzania's media scene". Latest East African & Bongo Flava Music, Songs & Video - Notjustok (kwa American English). 2024-09-10. Iliwekwa mnamo 2024-09-12.
  7. Agnes Opondo (2023-12-06). "Unkut Hiphop Awards Unveil 2023 Nomination Roster". KenyanVibe (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-09-12.