Salama Jabir

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Salama Zalhata Jabir (alizaliwa 1 Oktoba 1980) ni mtangazaji wa vipindi vya televisheni kutoka Tanzania[1]—hasa katika televisheni ya East Africa.[2]

Alizaliwa kwenye familia ya watoto tisa [3].

Hapo awali, alipata kuwa mtangazaji wa kipindi cha MkasiTv, kilichobuniwa na A.Y. Kipindi kilikuwa kinarushwa kupitia EATV—ambapo ndani yake wanahoji watu mbalimbali maarufu hadi hapo baadaye walipoamua kukiweka katika idhaa ya YouTube mnamo tarehe 1 Novemba 2011[4].

Salama pia ni jaji katika mashindano ya kutafuta vipaji vya wanamuziki yaitwayo Bongo Star Search akionekana kuwa ni jaji asemaye ukweli kwa wanaosailiwa[5].

Mafanikio[hariri | hariri chanzo]

Salama Jabir amepata mafanikio yafuatayo katika tasnia ya utangazaji na uanzishaji wa vipindi vya televisheni.

Mtangazaji mwanzilishi wa Planet Bongo[hariri | hariri chanzo]

Ni mtanganzaji na mwanzilishi wa kipindi cha televisheni cha Planet Bongo kinachorushwa na televisheni ya EATV [6] kilichoongeza ubora wa muziki wa Bongo Flava kwa upande wa utayarishaji wa video. Kabla ya kipindi hiki, wengi hawakuwa wanazingatia ubora wa kazi, lakini kupitia Salama walijitahidi sana kuboresha kazi zao kwa upande wa video ili wasijekunangwa naye.

Mtangazaji mwanzilishi wa Mkasi[hariri | hariri chanzo]

Amefanikiwa kuanzisha na kutanga katika kipindi cha televisheni cha Mkasi katika televisheni ya EATV. Baadae,baada ya kuacha kurushwa kwa kipindi hiki katika televisheni ya EATV Salama Jabir alianzisha chaneli ya Youtube yenye jina la MkasiTV yenye wateja 123638 mpaka makala hii ilipoahaririwa [7]

Mtangazaji wa kipindi cha Shabiki[hariri | hariri chanzo]

Mtangazaji wa kipindi cha televisheni cha Shabiki kinachorushwa katika televisheni ya EATV kinachohusu michezo na mashabiki wakihusishwa na timu baada na kabla ya timuzao kucheza.< [8]

Mtangazaji wa kipindi Ngaz kwa Ngaz[hariri | hariri chanzo]

Salama pia amefanikiwa kutangaza kipind cha televisheni cha Ngaz kwa Ngaz kinachorushwa na EATV .< [9]

Jaji wa Bongo Star Search[hariri | hariri chanzo]

Salama Jabir pia amekuwa akishiriki kama jaji katika mashindano ya kuibua vipaji vya wanamuziki yaitwayo Bongo Star Search

Mwanzilishi wa MkasiTV[hariri | hariri chanzo]

Amefanikiwa kuanzisha kampuni ya MkasiTV akishirikiana na AY na Josh Murunga[10]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Salama Jabir kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.