Reni Folawiyo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Reni Folawiyo ni mwanasheria, mwanamitindo na mfanyabiashara wa Nigeria, mwanzilishi wa Alara, duka la kwanza la mavazi na mitindo ghali Afrika Magharibi[1][2] lililobuniwa na masanifu majengo mwenye asili ya Uingereza na Ghana, David Adjaye[3] Anamiliki NOK na bustani ya NOK kukuza ladha ya kiafrika.[4]

Maisha ya Awali na Elimu[hariri | hariri chanzo]

Folawiyo alizaliwa London akiwa ni mtoto wa hayati Chifu Lateef Adegbite, aliyekua mwanasheria mkuu wa Nigeria na Katibu mkuu wa Baraza kuu la Uislam Nigeria [5] na alikulia Abeokuta, jimbo la Ogun, Nigeria.[6]

Alisomea sheria ya biashara katika chuo kikuu cha Warwick, Uingereza na alirudi Nigeria kufanyia mazoezi katika shirika la sheria la baba yake.[7]

Maisha Binafsi[hariri | hariri chanzo]

Aliolewa na mfanyabiashara wa Kinigeria Tunde Folawiyo mwaka 1989 na wamebahatika kupata watoto wawili, Faridah and Fuaad.[8]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Reni Folawiyo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.