Reinilde, Grimoaldi na Gondolfi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Reinilde akiwa amevaa kihija kadiri ya Maestro wa Elsloo, 1530 hivi.

Reinilde (pia: Reinhild, Rainelde n.k.; Condacum, leo nchini Ufaransa au Ubelgiji, 630 hivi; Saintes[1], Hainault, leo nchini Ubelgiji, 700 hivi) alikuwa mwanamke bikira wa ukoo wa kifalme, binti wa mtakatifu Amalberga wa Maubeuge.

Baada ya kuhiji Yerusalemu[2] alijitosa katika matendo ya huruma[3] hadi alipokatwa kichwa na Wahunni pamoja na shemasi Grimoaldi na mtumishi wake Gondolfi.

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 16 Julai[4]..

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Tubize. Communes of Brabant Wallon. Expatriate Online: Your Bookmark to Belgium. Jalada kutoka ya awali juu ya 2006-11-12. Iliwekwa mnamo 2007-02-21.
  2. Vita Reineldis, Acta Sanctorum, Julii IV, 173-178.
  3. Rabenstein, Katherine (July 1998). Reineldis. Saints O' the Day for July 16. Jalada kutoka ya awali juu ya February 6, 2007. Iliwekwa mnamo 2012-02-23.
  4. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.