Ram Prasad Bismil
Mandhari
Ram Prasad Bismil (11 Juni 1897 – 19 Disemba 1927) alikuwa mwanamapinduzi wa India aliyeshiriki katika njama maarufu za Mainpuri mwaka 1918, na Kakori mwaka 1925. Alikuwa mpiganiauhuru dhidi ya wakoloni wa serikali ya Uingereza, pia alikuwa mshairi mzalendo aliyeandika katika lugha ya Kiurdu akitumia lakabu ya Ram, Agyat na Bismil, lakini alijulikana zaidi kama "Bismil".
Bismil alikuwa mmoja wa waasisi wa chama cha kimapinduzi cha Hindustan Republican Association, alisifiwa zaidi na Bhagat Singh[1] kama mshairi gwiji wa Kiurdu na Kihindi ambaye alitafsiri vitabu katika lugha za Kiingereza na Kibengali.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ram Prasad Bismil kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |