Raúl Blanco

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Raúl Blanco (alizaliwa 27 Juni 1977) ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Real Madrid.

Anajulikana kama mchezaji muhimu wa muda wote katika historia ya timu ya klabu ya Real Madrid. Akiwa Real Madrid Raul alifanikiwa kuchukua makombe sita ya ligi kuu ya Uhispania,matatu ya UEFA Champions League na UEFA super cup.

Katika historia ya wafungaji bora wa ligi kuu ya Uhispania na mfungaji wa tano akiwa nyuma ya Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Telmo Zarra na Hugo Sanchez.

Amefanikiwa kutajwa kuwa mshambuliaji bora wa UEFA mara tatu na amefanikiwa kuchukua mara tano tuzo za mchezaji bora wa mwaka ikiwa ni mwaka 1997, 1999, 2000, 2001 na 2002.

Raul alistaafu soka mwaka 2015.

Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Raúl Blanco kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

.