Protista
Protista (kutoka Kiingereza "Protist") ni kundi la viumbehai wadogo sana, yaani vidubini ambao huwa na seli moja au chache tu. Mara nyingi hawaonekani kwa macho tu ila kwa hadubini tu, isipokuwa wakitokea kwa uwingi mkubwa.
Ni kundi lisilo na umoja, ila ndani yake hupangwa kiumbe yeyote wa jamii eukaryota asiye mnyama, wala mmea wala uyoga.
Zamani walihesabiwa kama himaya ya pekee ndani ya eukaryota lakini siku hizi hujumlishwa pamoja na himaya mbalimbali. Hapo pana protoktista ambao mifano yao ni: algae (viani), amiba na aina za kuvu.
Jina la Protista lilibuniwa na Ernst Haeckel mnamo 1866. Jina hilo linakusanya vidubini wenye tabia tofautitofauti, pamoja na wenye uwezo wa kujenga lishe yao kwa njia ya usanisinuru na wengine zinazotegemea mata ogania kama lishe.
Walio wengi huishi baharini au ndani ya viumbe wengine; kwa hiyo pengine ni chanzo cha magonjwa. Protisti wengi ni sehemu ya planktoni na hivyo ni muhimu sana kwa ekolojia ya uhai duniani.
Protista wachache wanasababisha magonjwa, kwa mfano protista anayejulikana kwa jina la Plasmodium falciparum inasababisha malaria; ugonjwa wa malale unatokana na protista ya trypanosoma brucei.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Protista kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |