Protista

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Protista

Protista ni kundi la viumbehai vidogo sana yaani vidubini ambavyo huwa na seli moja au seli chache tu. Mara nyingi havionekani kwa jicho tupu bali kwa hadubini tu isipokuwa zikitokea kwa uwingi mkubwa. Jina la Protista lilibuniwa na Ernst Haeckel mnanmo 1866.

Mifano ya protista ni algae (viani), amiba na aina za kuvu. Vilivyo vingi huishi baharini au ndani ya viumbe vingine; kwa hiyo vingine vinaonekana kama chanzo cha magonjwa. Protisti nyingi ni sehemu a planktoni na hivyo muhimu sana kwa ekolojia ya uhai duniani.

Zamani vilihesabiwa kama himaya ya pekee ndani ya eukaryota lakini siku hizi hujumlishwa pamoja na himaya mbalimbali. Jina hili linakusanya vidubini vyenye tabia tofautitofauti, pamoja na vyenye uwezo wa kujenga lishe yao kwa njia ya usanisinuru na nyingine zinazotegemea mata ogania kama lishe.


Protisti chache zinasababisha magonjwa kwa mfano protisti anayejulikana kwa jina la Plasmodium falciparum inasababisha malaria;ugonjwa wa malale unatokana na protisti ya trypanosoma brucei.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]