Nenda kwa yaliyomo

Prison Break

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Prison Break

Prison Break Msimu wa 3
Aina Maigizo, Kutisha, Aksheni
Nyota Washiriki wa Msimu wa 4:
Dominic Purcell
Wentworth Miller
Michael Rapaport
Amaury Nolasco
Robert Knepper
Jodi Lyn O'Keefe
With Sarah Wayne Callies
And William Fichtner
Nchi inayotoka Marekani
Lugha Kiingereza
Ina misimu 4
Ina sehemu Chicago, Illinois
Joliet, Illinois
Dallas, Texas
Los Angeles, California (Orodha ya sehemu)
Utayarishaji
Watayarishaji
wakuu
Marty Adelstein (2005-)
Neal H. Moritz (2005-)
Dawn Olmstead (2005-)
Brett Ratner (2005-)
Paul Scheuring (2005-)
Matt Olmstead (2005-)
Kevin Hooks (2006-)
Michael Pavone (2005)
Mtayarishaji
msaidizi
Zack Estrin (2005-)
Nick Santora (2005-)
Michael W. Watkins (2005)
Steve Beers (2005)
Mshauri mtayarishaji:
Marti Noxon (2005)
Watayarishaji wengineo:
Carlos Morales (2005-)
Msimamizi wa utayarishaji:
Karyn Usher (2005-)
Mtayarishaji mwenzi:
Ellen Marie Blum (2005-)
Agatha Aro Warren (2005-)
Sehemu Chicago, Illinois
Joliet, Illinois
Dallas, Texas
Los Angeles, California
Muda makisio ni dk. 42
Urushaji wa matangazo
Kituo FOX
Inarushwa na 29 Agosti 2005 - hadi leo
Viungo vya nje
Profaili ya IMDb
Muhtasari wa TV.com

Prison Break ni mfululizo wa kipindi cha televisheni cha Kimarekani, ambacho kilianza kurushwa hewani tangu mnamo tar. 29 Agosti 2005 na kituo cha TV cha Fox Broadcasting Company.[1]

Mfululizo una husisha ndugu wawili; mmoja ambaye yupo amehukumiwa kifo kwa kosa ambalo hakuhusika nalo, mwingine, mjanja, ambaye amepanga mpango madhubuti wa kuweza kumtorosha ndugu yake jela.

Mfululizo umetungwa na Paul Scheuring, kipindi kimetayarishwa na Adelstein-Parouse Productions kwa ushirikiano wa Original Television na 20th Century Fox Television.

Mtayarishi mkuu anayetayarisha sasa ni Scheuring (pia ndiyo Mtunzi Mkuu), Matt Olmstead (Mtunzi-Msaidizi), Kevin Hooks, Marty Adelstein, Dawn Olmstead, Neal H. Moritz, na Brett Ratner. Kibwagizo cha mfululizo huu kimeundwa na Ramin Djawadi, na kilitunukiwa Tuzo ya Primetime Emmy Award kwa mwaka wa 2006.[2]

Muhtsari wa mfululizo huu

[hariri | hariri chanzo]

Ufupisho wa Msimu wa Kwanza

[hariri | hariri chanzo]

Msimu huu una vipengele 22 na ulianza kurushwa hewani kwa mara ya kwanza 29 Agosti 2006 kupitia Fox Network, Marekani. Lincoln Burrows (Dominic Purcell) anatuhumiwa kumuua Terrence Steadman ( Jeff Perry), kaka wa makamu wa rais wa Marekani. Kutokana na kuwepo ushahidi mzito katika tuhuma hizo, Lincoln anahukumiwa kifo na anapelekwa katika gereza la Fox River State kusubiri hatma yake.

Kaka yake Lincoln, mhandisi machachari Michael Sofield (Wentworth Miller), anaamini kuwa kaka yake hana hatia na anasuka mpango wa kumtorosha. Anafanya tukio la kupora benki moja ili afungwe katika gereza la Fox River kwa kujitakia, huku akishindana na muda katika kuhakikisha anakabiliana na vizuizi na anajiunga na wafungwa na wafanyakazi wa gereza katika kuhakikisha anafanikiwa kumtorosha kaka yake. Wakisaidiwa na rafiki yao wa muda mrefu Veronica Donovan (Robin Tunney), anayeanza kuchunguza hujuma iliyotumika kumuingiza Lincoln jela.

Hata hivyo wanakwazwa na makachero wasiojulikana, wanaotokea katika kundi linalojulikana kama The Company. Hiyo The Company ndiyo hasa inayohusika na sakata zima la kumpaka matope Lincoln na bado haijajulikana kwa nini.

Hatimaye ndugu wawili, pamoja na wafungwa wengine sita, Sucre (Amaury Nolasco), T-Bag (Robert Knepper), C-Note (Rockmond Dunbar), Tweener (Lane Garrison), Abruzzi (Peter Stomare), na Haywire (Silas Weir Mitchell) ambao wanakuja kujulikana kama Fox River Eight wanafanikiwa kutororka mwishoni mwa msimu.

Ufupisho wa Msimu wa Pili

[hariri | hariri chanzo]

Msimu huu una vipengele 22 na ulianza rasmi kurushwa hewani kuanzia 21 Agosti 2006 hadi 2 Aprili 2007 kupitia Fox Network, Marekani. Msimu unaanzia masaa nane baada ya kutoroka, ukielemea hasa kwa wale waliotoroka. Mtunzi wa tamthilia, Paul Scheuring anaupachika msimu wa pili jina la "The Fugitive times eight".

Wakimbizi wanatawanyika na wanafanya safari wakiikatisha nchi huku vyombo vya dola vikiwa nyuma yao na kila mmoja akiwa na lengo lake. Brad Bellick (Wade Williams) anafukuzwa kazi gerezani alipokuwa akifanya kazi kama askari katika msimu wa kwanza na anawafukuza wakimbizi mwenyewe ili kupata zawadi nono iliyowekwa kwa atakayesaidia kuwakamata wahalifu hao.

Baadhi ya wakimbizi wanajiunga kufuatilia pesa zilizofichwa kitambo na mfungwa mwenzao. T-Bag anafanikiwa kuondoka na pesa hizo na ndugu wanatumia msimu mzima kumsaka kutokana na hizo pesa na vilevile Scofield anajilaumu kwa kumpa uhuru muuaji.

Kachero wa FBI Alexander Mahone (William Fichtner) anachaguliwa kuwafuatilia na kuwanasa wakimbizi wote nane, lakini inakuja kujulikana kuwa na yeye ni mshirika wa The Company; The Company inawataka watu wote nane, hasa - kumuua Lincoln.

Baadhi ya waliotoroka wanauawa na kukamatwa, lakini ndugu hawa wanafanikiwa kuingia Panama. Mwishoni mwa msimu, ushahidi wa aliyekuwa kachero wa CIA, aliyewahi kuitumikia The Company unamuweka huru Lincoln wakati Michael, T-Bag na Mahone wanakamatwa na kufungwa kwenye gereza la SONA ambapo wanamkuta Bellick aliyetiwa kifungoni siku kadhaa kabla.

Ufupisho wa Msimu wa wa Tatu

[hariri | hariri chanzo]

Msimu huu una vipengele kumi na moja na kwa mara ya kwanza ulirushwa hewani kuanzia 17 Septemba 2007 hadi Febuary 18, 2008 kupitia Fox Network, Marekani. Msimu unaendelea kwa kuwafuatilia wote Michael akiwa ndani ya Sona na Lincoln akiwa nje.

Sona ni jela inayoendeshwa na wafungwa wenyewe huku gereza likilindwa na maaskari kwa nje tu. Burrows anawahiwa na The Company ambao wanamshikilia mwanawe L. J. (Marshal Allman) na Sara Tancredi (Sarah Wayne Callies), msichana aliye kwenye mapenzi mazito na Michael, na wanamwambia kuwa wanachotaka wao ni Michael kufanya kazi ya kumtorosha James Whistler (Chris Vance) kutoka Sona.

Msimu unaendelea ukiwaonesha Michael na Whistler wakiwa katika harakati za kusuka mpango wa kutoroka. Michael anakabiliana na shinikizo huku Lincoln akikabiliana na mwanaharakati wa The Company Gretchen Morgan (Jodi Lyn O’Keefe). Sucre anapata kazi gerezani ili kumsaidia Michael na mpango wake wa kutoroka.

Michael anashindwa kufanikisha mpango huo katika muda waliopangiana na Lincoln anajaribu kutumia mbinu mbadala, Morgan ‘anamchinja Sara’ na anamtumia Lincoln kichwa ili kumuonya. Msimu unaishia kwa vijana kufanikiwa kutoroka pamoja na Mahone kwa kuwazunguka T-Bag na Bellick.

Sucre anatambuliwa na askari wa gereza na anatupwa Sona baada tu ya wenzake kutoroka. Wanabadilishana L. J. kwa Whistler na Michael anaonekana akimfuatilia Gretchen ili kulipa kisasi kutokana na ‘kifo cha Sara’.

Ufupisho wa Msimu wa Nne

[hariri | hariri chanzo]
Amaury Nolasco, Robert Knepper, Sarah Wayne Callies, Wentworth Miller na Matt Olmstead kunanko mwaka wa 2008.

Msimu huu ulinza kuruka hewani rasmi mnamo 1 Septemba 2008 na unaendelea kutoka ule wa tatu. Michael anataka kulipa kisasi kutokana na kifo cha Sara na anagundua kuwa yupo hai na kichwa alichopewa Lincoln ni cha mtu mwingine.

Michael pia anagundua ukweli hasa juu ya Whistler kuwa alikuwa akishirikiana kwa ukaribu na Mahone kuiangusha The Company. Whistler anauliwa na muuaji wa The Company.

Inagundulika kuwa wafungwa waligoma kule Sona na Bellick, T-Bag na Sucre wakafanikiwa kutoroka. Donald Self (Michael Rapaport), kachero kutoka kamati inayojihusisha na mambo ya ndani anawaunganisha Michael na Lincoln, vilevile Sucre, Bellick na Mahone kutoa msaada kuiangusha The Company kwa mkataba wa kuwa huru endapo watafanikisha zoezi hilo.

Sara pia anajiunga kwenye kundi baada ya kutoroka kwenye mikono ya Gretchen kitu ambacho kimesababisha Gretchen kuwekwa kizuizini na The Company kutokana na kushindwa kutimiza wajibu wake, na Roland (James Hiroyuki Liao), kijana machachari katika mambo ya computer anayeingizwa kwenye timu baada ya kufungwa kwa kosa la kuiba utambulisho wa mtu mwingine.

Kwa pamoja wanatengeza mpango wa kupata taarifa kutoka The Company ambazo zitawasaidia kuiangusha hiyo The Company. Wakati huo Wyatt (Cress Williams), kachero wa The Company, anawafuatilia Michael na Lincoln ili kuwaua na T-Bag anaelekea kaskazini mwa Marekani akiwa na kitabu ‘Birds’ book pamoja nae. Yupo kwenye harakati za kuiba mpango wa Whistler.

  1. Fox Broadcasting Company, Prison Break show info Archived 10 Mei 2008 at the Wayback Machine., Prison Break official site. Retrieved on 13 Septemba 2007.
  2. Emmy nominations in all categories Archived 26 Januari 2007 at the Wayback Machine. Associated Press. 6 Julai 2006. Retrieved on 10 Oktoba 2006.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: