Nenda kwa yaliyomo

Pompei

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Altare mbele ya nyumba ya Herculaneum iliyofunuliwa.

Pompei ni mji wa mkoa wa Campania, Italia Kusini wenye wakazi 25,440 (sensa ya mwaka 2011) uliopo karibu na jiji la Napoli.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Pompei (kwa Kilatini: Pompeii) ilikuwa mji wa Roma ya Kale katika Italia ya kusini karibu na mji wa Napoli ya leo.

Mji ulianzishwa mnamo karne ya 9 KK: ndipo jamii zilipoanza kuishi katika huko na kuanzisha makazi na kufanya kazi kwa bidii na kuujenga mji.

Mlipuko wa volkeno Vesuvio uliotokea tarehe 24 Agosti 79 BK ulifunika mji wote pamoja na mji wa jirani Herkulaneo kwa ganda nene la majivu na zaha (lava) la mita sita. Wakati volikano inalipuka katika mji huo, tayari ulikuwa umejengeka sana. Watu wengi waliuawa na wachache waliweza kukimbia kwani majivu, joto, vumbi lililotanda liliwapa kizuizi cha kukimbia na kujiokoa na familia zao..

Kuna taarifa kamili ya uharibifu wa Pompei kwa sababu mwandishi Mroma Plinio Kijana alishuhudia yaliyotokea akiwa kwenye meli baharini karibu na mlima na mji wa Pompei; kuna barua kadhaa ambamo alieleza alichoona. Aliandika kuhusu mlipuko huo na kutoa ufafanuzi juu ya janga hilo, alisema katika jarida lake "watu wengi walipoteza uhai katika tukio hilo na ni nusu ya mji huo wa Pompei, japo kuna waliofanikiwa kukimbia na kuokoka; watoto na wanawake ndio waliodhurika zaidi, pia wazee na wasiojiweza".

Tangu karne ya 18 (1748) maghofu ya Pompei yalifunuliwa tena polepole. Nyumba pamoja na vifaa vilivyohifadhiwa vizuri sana chini ya majivu zinaleta picha nzuri ya maisha ya Roma ya Kale. Hivyo mji huo umeweka kama historia na kumbukumbu na historia ya Waroma. Leo hii mji wa kihistoria unatembelewa na watalii zaidi ya milioni 7 kwa mwaka, wakiwemo Waitalia wa watu kutoka nchi nyingine. Imo katika orodha ya mahali pa Urithi wa Dunia ya UNESCO.

Pamoja na yote, mji wa Pompei umejengeka upya na una wakazi zaidi ya 25,000.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Pompei kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.