Nenda kwa yaliyomo

Kwera

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ploceus)
Kwera
Kwera nguya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Ploceidae (Ndege walio na mnasaba na kwera)
Ngazi za chini

Jenasi 3:

Kwera ni ndege wadogo wa jenasi Anaplectes, Brachycope na Ploceus katika familia Ploceidae. Takriban spishi zote zinatokea Afrika, lakini spishi tano zinatokea Asia. Rangi kuu ya ndege hawa ni njano, isipokuwa kwera kichwa-chekundu, kwera michirizi, kwera kahawiachekundu na kwera mweusi. Mara nyingi kichwa au uso ni nyeusi. Spishi bila nyeusi kichwani huitwa mnana. Spishi nyingine huitwa chambogo.

Ndege hawa hula mbegu hasa lakini wadudu pia, hususa makinda. Spishi hizi hulifuma tago lao kwa majani ya manyasi na hulining'inizia kitawi. Matago yao hupatikana katika makundi makubwa. Jike huyataga mayai 2-4.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za Asia

[hariri | hariri chanzo]