Petro wa Poitiers

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Petro wa Poitiers (Poitiers, Akwitania, leo nchini Ufaransa, karne ya 11 - Chauvigny, 4 Aprili 1115) alikuwa askofu wa mji huo (kwa Kilatini Pictavium) kuanzia mwaka 1087 hadi alipofukuzwa kinyume cha haki kwa kukaripia watawala waovu.

Ni maarufu kwa kusaidia uanzishwaji na uthibitishwaji wa Utawa wa Fontevrault[1].

Tangu zamani anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe aliyofariki dunia [2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.