Nenda kwa yaliyomo

Pimbi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Perere)
Pimbi
Pimbi mkubwa kwenye Mlima Kenya (Procavia capensis)
Pimbi mkubwa kwenye Mlima Kenya (Procavia capensis)
Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Eukaryota
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda ya juu: Afrotheria
Oda: Hyracoidea (Wanyama kama pimbi)
Familia: Procaviidae (Wanyama walio na mnasaba na pimbi)
Thomas, 1892
Ngazi za chini

Jenasi 3, spishi 4:

Pimbi, kwanga, perere au wibari ni wanyama wadogo wa familia Procaviidae. Jina la kwanga litumika kwa jenasi Heterohyrax na perere na wibari yatumika kwa jenasi Dendrohyrax. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara na Mashariki ya Kati, mara nyingi katika maeneo makavu na yenye miamba mingi. Spishi zote ni nene zenye mkia mfupi na manyoya mazito. Miguu yao ina vitakia vyenye ngozi nene na tezi nyingi za jasho ambavyo vinawasaidia kupanda miamba na miti. Rangi yao ni kijivu, kahawia au hudhurungi. Hula majani ya manyasi, ya mimea na ya miti.

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.