Shomoro
Mandhari
(Elekezwa kutoka Passer)
Shomoro ni ndege wadogo wa jenasi Passer katika familia ya Passeridae ambao wana rangi ya nyeusi, nyeupe, majivu na kahawia. Ndege hawa huitwa korobindo pia, lakini jina hili litumike afadhali kwa kuita ndege wa jenasi Petronia. Shomoro wenye kichwa kijivu huitwa jurawa. Ndege hawa wana domo fupi na nene lifaalo kula mbegu, lakini hula wadudu wadogo pia hasa wanapokuwa vifaranga. Kwa asili shomoro wanatokea Ulaya, Afrika na Asia, lakini watu wamewaletea Australia na Marekani.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Passer castanopterus, Shomoro Somali (Somali Sparrow)
- Passer cordofanicus, Shomoro wa Kordofani (Kordofan Rufous Sparrow)
- Passer diffusus, Shomoro Kusi au Jurawa Kusi (Southern Grey-headed Sparrow)
- Passer domesticus, Shomoro-kaya (House Sparrow)
- Passer eminibey, Shomoro Kahawianyekundu (Chestnut Sparrow)
- Passer euchlorus, Shomoro Manjano Arabi (Arabian Golden Sparrow)
- Passer gongonensis, Jurawa Domo-nene (Parrot-billed Sparrow)
- Passer griseus, Shomoro Jurawa au Jurawa (Grey-headed Sparrow)
- P. g. ugandae, Jurawa wa Uganda (Uganda Sparrow)
- Passer hemileucus, Shomoro wa Abdel Kuri (Abd al-Kuri Sparrow)
- Passer hispaniolensis, Shomoro wa Hispania (Spanish Sparrow)
- Passer iagoensis, Shomoro wa Cabo Verde (Iago or Cape Verde Sparrow)
- Passer insularis, Shomoro wa Socotra (Socotra Sparrow)
- Passer luteus, Shomoro Manjano (Sudan Golden Sparrow)
- Passer melanurus, Shomoro Uso-mweusi (Cape Sparrow or Mossie)
- Passer motitensis, Shomoro Mkubwa (Great Sparrow)
- Passer rufocinctus, Shomoro Mwekundu (Kenya Sparrow)
- Passer shelleyi, Shomoro wa Shelley (Shelley's Sparrow)
- Passer simplex, Shomoro-jangwa (Desert Sparrow)
- Passer suahelicus, Jurawa Swahili (Swahili Sparrow)
- Passer swainsonii, Jurawa wa Swainson (Swainson's Sparrow)
Spishi za Ulaya na Asia
[hariri | hariri chanzo]- Passer ammodendri (Saxaul Sparrow)
- Passer cinnamomeus (Cinnamon or Russet Sparrow)
- Passer flaveolus (Pegu or Plain-backed Sparrow)
- Passer italiae (Italian Sparrow) - kwa asili chotara ya P. domesticus na P. hispaniolensis
- Passer moabiticus (Dead Sea Sparrow)
- Passer montanus (Tree Sparrow)
- Passer pyrrhonotus (Sind Sparrow)
- Passer zarudnyi (Asian Desert Sparrow) - huainishwa pia kama nususpishi ya P. simplex
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Shomoro-kaya
-
Jurawa
-
Shomoro wa Hispania
-
Shomoro manjano
-
Shomoro uso-mweusi
-
Shomoro-jangwa
-
Jurawa Swahili
-
Saxaul sparrow
-
Cinnamon sparrow
-
Tree sparrow
-
Sind sparrow