Bata mkia-ngumu
Mandhari
(Elekezwa kutoka Oxyura)
Bata mkia-ngumu | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 4, spishi 10:
|
Mabata mkia-ngumu ni ndege wa maji wa nusufamilia Oxyurinae katika familia Anatidae. Manyoya ya mkia wao ni makavu na yametandawaa mara nyingi. Rangi ya dume ni kahawia au kahawiachekundu na domo lake lililovimba msingini ni buluu; jike ni mweusi au kijivu wenye domo la rangi ile ile. Spishi hizi huzamia kabisa ili kutafuta chakula. Hula mimea na invertebrata ya maji. Miguu yao iko nyuma sana, kama ile ya mabata wazamaji, ili kujisogeza mbele vizuri ndani ya maji. Kwa sababu hiyo hawawezi kutembea vizuri. Hujenga tago lao ndani ya uoto mzito wa maji. Jike huyataga mayai 3-8, lakini pengine hadi mayai 12 yanapatikana kwa sababu jike mwingine ameongezea mayai yake.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Oxyura jamaicensis, Bata Uso-mweupe (Ruddy Duck) imewasilishwa
- Oxyura leucocephala, Bata Kichwa-cheupe (White-headed Duck)
- Oxyura maccoa, Bata Makoa (Maccoa Duck)
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Biziura lobata (Musk Duck)
- Heteronetta atricapilla (Black-headed Duck)
- Nomonyx dominicus (Masked Duck)
- Oxyura australis (Blue-billed Duck)
- Oxyura ferruginea (Andean Duck)
- Oxyura vantetsi (New Zealand Stiff-tailed Duck imekwisha sasa (miaka 1500)
- Oxyura vittata (Argentine Blue-bill)
Spishi ya kabla ya historia
[hariri | hariri chanzo]- Biziura delautouri (De Lautour's or New Zealand Musk Duck, Holocene ya New Zealand)
- Tirarinetta kanunka (Piocene ya Australia Kusi)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Bata uso-mweupe
-
Bata makoa
-
Musk duck
-
Black-headed duck
-
Masked duck
-
Blue-billed duck
-
Andean duck
-
Argentine blue-bill